Wabunifu tisa kutoka Tanzania na taasisi moja isiyo ya kiserikali, Ubongo Kids, wapatiwa ruzuku ili kuwezesha utekelezaji wa ubunifu wao kupitia mpango wa Data for Local Impact Innovation Challenge (DLIIC) inayofadhiliwa na Mpango wa Dharura wa Rais wa Serikali ya Marekani unaojihusisha na masuala ya Ukimwi (PEPFAR) chini ya Ushirikiano wa (DCLI) wanaosimamiwa na taasisi ya kimataifa ya Millennium Challenge Cooperation (MCC). Kwa kuteuliwa washindi hao watapata fedha kuanzia dola za Marekani 10,000 hadi 25,000 (watu binafsi) na dola 100,000 (kwa shirika) pamoja na msaada wa kiufundi na ushauri ili waweze kutekeleza aina mbalimbali za ufumbuzi wa matatizo katika jamii.
Mnamo Oktoba 11 mwaka huu , DLIIC itasherehekea na wabunifu hawa kama sehemu ya sikukuu ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike iliyoanzishwa mwaka huu na Umoja wa Mataifa ikiwa na kauli mbiu “Nguvu ya Mtoto wa kike ikiwa na malengo ya hadi mwaka 2030”.
Dirisha la kwanza la DLIIC lilifunguliwa Oktoba 2016 likiwa na mapendekezo ya matumizi ya takwimu/Data ili kuweza kupata matokeo bora ya afya na kusaidia katika vipaumbele vya afya vya Serikali ya Tanzania. Dirisha hili la pili pia lilizingatia vipaumbele vya afya vya Serikali ya Tanzania, na hasa kusaidia mipango ya kimkakati ya PEPFAR ili kushughulikia maambukizi ya VVU / UKIMWI kwa watoto wa kike waliopevuka na wasichana vijana (AGYW), ushirikiano unaojulikana kama DREAMS (Uamuzi, Ufanisi, Uwezeshwaji, epuka UKIMWI , Maelekezo, na Salama).
Ushirikiano wa DREAMS husaidia wasichana waliopevuka na wanawake vijana walio katika mazingira hatarishi wenye umri kati ya miaka 10-24, ukilenga zaidi kwa wale wenye umri wa miaka 15 hadi 24. Kundi hilo ndilo liko katika mazingira hatarishi mara mbili nukta tano zaidi ya kuambukizwa VVU / Ukimwi kuliko wenzao wa kiume. Ushirikiano huu wa DREAMS unalengo la kupunguza hatari hii kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana na pia kupunguza maambukizi mapya ya VVU kati ya vijana hao wenye umri huo wa kati ya miaka 15-24 kwa asilimia 40 kupitia jitihada zenye vielelezo maalumu unaozingatia idadi ya watu katika makundi manne ambayo: wanawake vijana, watoa huduma, wapenzi wao, na washirika wao katika jamii. Hatua hizi zimeshibitishwa kupunguza tabia zinazosababisha uenezaji wa VVU na unyanyasaji wa kijinsia (GBV).
Dirisha la pili la liliwalika waendelezaji wa ndani ili kupata ubunifu mpya, teknolojia, na taratibu zinazozotumia takwimu ili kushughulikia masuala yanayowakabili wasichana na wanawake vijana na kuchangia kupunguza maambukizi ya VVU.
Mapendekezo yaliyoshinda yalijumuisha ubinifu wa kupata suluhisho katika maeneo yafuatayo:
- Kuongezeka kwa ushiriki wa wanaume katika kujenga mazingira salama na kinga kwa Wasichana waliopevuka na wanawake vijana;
- Kupunguza Uachaji wa shule ambao unapunguza fursa muhimu kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana;
- Kupanua uwezeshaji wa kiuchumi na mikakati ya kuongeza uhuru wa kiuchumi kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana; na
- Kuongeza uongozaji kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana na ufanyaji wa maamuzi katika kupambana na VVU.
Katika maeneo hayo mapendekezo kumi yalichaguliwa kutoka katika maombi 190 baada ya kupitiwa na jopo huru la la wajasiliamali wa kitanzania waliobobea katika masuala ya afya, na wataalamu wa jinsia.
Mapendekezo yalitakiwa kuzalisha au kutumia takwimu wazi na ziwe zimefanyiwa kazi katika kipindi cha ndani ya miezi mitatu hadi sita na kuzingatia masuala yanayowakabili vijana, wasicaha wadogo na jamii zilizopuuzwa. Ubunifu huo pia ulitakiwa kulenga angalau moja ya wilaya 89 ambazo zinapewa vipaumbele chini ya mpango wa PEPFAR 2017 Tanzanian Country Operational Plan (COP) au chini ya Mpango wa Mfuko wa Kimataifa ulioandaliwa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania. Mapendekezo yaliyoshinda, yameorodheshwa kwa kutaja viongozi wa timu na mada zao kuu, kama ifuatavyo;
Kuongezeka kwa usiriki wa wanaume katika kujenga mazingira salama na kinga kwa Wasichana waliopevuka na wanawake vijana;
- Leyla Liana Hamisi
- Mkata Nyoni
Kupunguza Uachaji wa shule ambao unapunguza fursa muhimu kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana;
- Husseni Kiranga
- Judith Leo
- Maria Dorin Shayo
- Wilson Mnyabwilo
Kupanua uwezeshaji wa kiuchumi na mikakati ya kuongeza uhuru wa kiuchumi kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana;
- Doreen Kessy – Ubongo Kids
Kuongeza uongozaji kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana na ufanyaji wa maamuzi katika kupambana na VVU.
- Asha Kombo
- Emila Msangi
- Musafiri Mbilinyi
“DLIIC ina lengo la kushiriki, kusaidia, na kuunganisha wabunifu wa Kitanzania, watengenezaji, wavumbuzi na kufadhili ili kila mmoja aweze kupata fursa za kufanya vitu tofauti vinavyoyakabili maisha ya watu,” alisema Agapiti Manday ambaye ni Meneja wa Programu wa DLIIC.
Alisema DLIIC imeandaliwa kimkakati na ili kuwashirikisha kikamilifu vijana katika matumizi yao ya takwimu/data na kuwajengea uwezo katika utumiaji wa data za kisayansi na kuchangia lengo la PEPFAR la kuwa na ushiriki mkubwa kwa wananchi nchini katika kudhibiti, na hatimaye kulitokomeza ugonjwa wa UKIMWI.
Washindi wataanza mafunzo yao mwezi Oktoba 2017, na watafanya kazi ya kutekeleza miradi yao ndani ya miezi mitatu hadi sita. Washindi hao watakuwa sehemu ya mpango wa ujasiriamali ambao utaimarisha ujuzi wao wa usimamizi wa miradi, biashara na watakuwa na uwezo wa kutumia data kisayansi. Jambo muhimu zaidi washindi hawa watasambaza maana halisi ya kupatikana ufumbuzi wa matatizo yanayokabili maisha ya jamii ya Kitanzania hasa wasichana waliopevuka na wanawake vijana.


Leave a Reply