Dirisha la kwanza la DLI Innovation Challenge lililenga mashirika na watu binafsi kutoka Tanzania nzima.
Uombaji wa ushiriki katika shindano hiulo ulianza kuanzia Oktoba 25 hadi Novemba 26 mwaka jana saa 6:00 usiku.
Dirisha hilo la kwanza liliwavutia waombaji wapatao 723 kutoka taasisi 190 ziulizosajiliwa na 533 kutoka kwa waombaji binafsi.
Hata hivyo ni taasisi 33 na watu binafsi 131 waliotimiza masharti ya uombaji.
Pia kati ya waombaji hao waliotimiza masharti ya uombaji ni taasisi 11 na watu binafsi 118
Baada ya kukamilika mchakato huyo jopo kutoka kwa wabunifu na wataalamu wa afya nchini Tanzania walikaa na kupitia masharti na vigezo yaliyoorodheshwa katika kitabu cha masharti kwa waombaji cha DLIIC.
Baada ya kupitia kitabu hicho na kujiridhisha, jopo hilo la majaji lilikaa na kuteua orodha ya washindi wa mwisho ambapo taasisi nne na watu binafsi 22 waliofanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo na kupata nafasi ya kutetea mapendekezo yao kwa majaji jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lilifanyika Desemba 3 mwaka jana katika Kitivo cha Takwimu cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (Co-ICT) na kuhudhuriwa na maofisa wa ngazi ya juu kutoka Mpango wa Changamoto za Millennium (MCC) na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR).
Nafasi yetu katika kuendesha mchakato huu? Watu ambao ni wavumbuzi na wabunifu ambao tulikutana katika Dirisha la kwanza la walitupa nguvu na kutuongezea msisimko katika utendaji wa kazi zetu.
Wakati wa mchakato wa kutafuta ushirikiano, timu yetu ya mradi ilikutana na waboreshaji wa ndani 688 ambapo katika idadi hiyo walikuwapo wanawake 124 katika vikao vya hana kwa hana vilivyofanyika katika vyuo vikuu na vyuo vikuu vya uvumbuzi ili kuweza kuwaeleza malengo ya mpango huu wa DLI.
Mbali na hao pia vilevile tuliweza kukutana na mamia kupitia katika vyombo vya habari vya kijamii ili kujadiliana kuhusu fursa hii na kujibu maswali yao kuhusu taasisi za nje na za ndani zinazoomba ruzuku kutoka DLIIC.
Kwa kupitia njia hii ya mazungumzo yalituwezesha kuwasaidia wale waliokuwa na maswali juu ya mpango huu, jinsi ya kujaza fomu ya maombi na kuwasilisha mawazo yao ambao matokeo yake yote unaweza kuyapata katika kurasa zetu za Facebook na Twitter .
Tunatarajia utaendelea kushirikiana nasi ili kuweza kuongeza nguvu katika mpango wa dirisha la pili ambao unatarajia kuja hivi karibuni mapema Machi 2017.
Leave a Reply