Washindi katika dirisha la kwanza

Steven Edward Mangowi

Steven Edward Mangowi

Huduma za Afya na Viwango vya Utumiaji (HSRS)

Nikiwa kama mboreshaji mwenye uzoefu, nataka kutumia maelezo ya kijiografia na viwango vinavyotokana na jamii ili kuwawezesha watumiaji wa kituo cha afya kupata huduma fulani na kujua ubora wa huduma hiyo kwa kutumia simu zao za mkononi.
Mimi pia nataka kutumia takwimu kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa za Tanzania (TFDA) ili kuwawezesha wagonjwa kuangalia kwamba madawa yanayopatikana yamesajiliwa nchini Tanzania.

Rose Peter Funja

Rose Peter Funja

Uachaji wa Shule Utokanao na Sababu za kiafya na Ufahamu mdogo wa ufuatiliaji wa Vihatarishi

Mimi nikiwa mwanamke na mhandisi, nataka kutumia uchambuzi wa kutabirika na mashine za kujifunzia ili niweze kuwasaidia Maofisa Mipango wa Wilaya kutabiri athari za bajeti ya elimu kwenye viwango vya uachaji shule kwa wasichana lengo likiwa ni kupunguza viwango vya uachaji shule kwa wasichana na kuwawezesha kupata elimu.

Rahim Abas Kiobya

Rahim Abas Kiobya

Geo-Afya (GIS in Healthcare Services)

Nikiwa kama mwanasayansi wa takwimu, nataka kuchanganya habari za kijiografia na takwimu zilizowazi ili kuonyesha kupangilia rasilimali za afya na magonjwa na mazingira yake ili tuweze kuboresha ufuatiliaji wa huduma za afya.

Rachel Samuel Nungu

Rachel Samuel Nungu

Mimi kama daktari, nataka kufanya kazi kama kiungo kati ya jamii na mamlaka za vituo vya afya. Ninataka kuwapa Watanzania sauti ya kushiriki maoni yao juu ya ubora wa huduma za afya wanazopokea, na pia waweze kutumia takwimu hizi ili kusaidia bodi za serikali zinazojihusisha na masuala ya afya katika uboreshaji huduma zake na kuwafanya watu waweze kuamini vituo vya afya na kupata huduma bora zaidi.

Mohammad Abdulghany Himidi Msoma

Mohammad Abdulghany Himidi Msoma

Health Loc

Nikiwa na asili ya Zanzibar, nataka kutumia takwimu zailizowazi ili kusaidia raia wenzangu (na watalii) kwenda katika hospitali na maduka ya madawa kwa muda muafaka wanapohitaji huduma za matibabu hivyo kwa kupitia mpango huu wataweza kufahamu mahali pa kwenda.

Lulu Said Ameir

Lulu Said Ameir

Be A Lady (Usimamizi wa Usafi wa Hedhi)

Kama mjasiriamali mdogo, mimi nataka kufunga mashine za utengenezaji wa pedi kwenye mashule ili kuwasaidia wasichana waliobarehe kupata pedi safi na za bei nafuu. Lakini pia nataka kukusanya takwimu ili kupata uthibitisho wa jinsi gani mashine hizi zimeweza kupunguza utoro wa wasichana utokanao na hedhi. Lengo si kuwa tu mjasiriamali lakini pia niweze kufikia lengo langu la kuwasaidia wasichana wenzangu na wanawake, sababu ili tatizo kubwa tunalokumbana nalo kila siku.

Joyce Samwel Msigwa

Joyce Samwel Msigwa

Doctor Fasta

Nikiwa mmoja kati ya watu waliopata shida katika kumpata mtaalam wa tatizo la kiafya, nataka kutumia teknolojia ya simu ya mkononi ili kuunganisha wataalamu wa afya (madaktari) na watu wanaohitaji huduma, hasa katika maeneo ya vijijini, ili Watanzania waweze kuunganishwa na huduma za afya wanazohitaji haraka na kwa urahisi.

Josephat Geoffrey Mandara

Josephat Geoffrey Mandara

Tausi Jukwaa

Nikiwa kama kaka, inaniumiza ninaposikia kuna baadhi ya wanafunzi wa kike hushindwa kuhudhuria masomo wanapokuwa katika siku zao.
Kutokana na tatizo hilo nataka kutumia jukwaa lakielektroniki katika kupeana taarifa kuhusu Usimamizi wa Usafi wakati wa Hedhi katika shule za sekondari ili kukuza uelewa juu ya usafi wakati wa hedhi, na tunaweza kupunguza idadi ya wasichana wanaoacha masomo kutokana na hedhi.

Jonathan Manyama Kifunda

Jonathan Manyama Kifunda

Usichana Wangu Kwanza

Kama mwanaharakati wa jamii, nataka kutumia takwimu ili kuendeleza Kitabu changu cha Usimamizi wa Usafi kipindi cha Hedhi (MPM) ili kuwaelimisha wasichana, wazazi, na walimu ili tuweze kuhamasisha mazungumzo ya wazi karibu na MPM na kuwasaidia kuelewa kwamba kipindi cha hedhi kwa mwanamke ni sifa; Si laana. Lengo ni hatimaye tuweze kuwarejesha wanawake na wasichana wadogo mashuleni na kupunguza ubaguzi unaosababishwa na hedhi.

Jackson Ilangali

Jackson Ilangali

Hospital Info System

Kama daktari kitaaluma, nataka kutumia teknolojia ya simu ili kuongeza ufikiaji wa habari unaopatikana kwenye Msajili wa Kituo cha Afya ili wagonjwa waweze kuuliza kwa SMS kuhusu aina za huduma zinazotolewa katika vituo vya afya vya karibu na kufanya maamuzi kuhusu mahali bora pa kwenda kwa ajili ya huduma iliyosahihi na bora.

George Elly Matto

George Elly Matto

AfyaBox

Kama mtafiti ambaye nataka kusaidia jamii yangu, nataka kutumia teknolojia ya simu ili kuwezesha upatikana wa taarifa sahihi kutoka kwa Msajili wa Kituo cha Afya na kuhakikisha zinapatikana kupitia simu zote za mkononi kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili ili kila mtu aweze kupata taarifa za vituo vya afya nchini Tanzania.

Bukhary Haruna Kibonajoro

Bukhary Haruna Kibonajoro

OKOA

Kama mbunifu mdogo na mjasiriamali katika sekta ya teknohama, nataka kutumia takwimu zenye ubora za huduma ya afya ili kutoa urahisi katika upatikanaji wa huduma bora za afya - hasa upatikanaji wa madawa kwa watu masikini ambao kwa kawaida hutafuta huduma katika vituo vya afya ili tuweze KUWAOKOA: Katika kuokoa muda, kuokoa pesa, kuokoa maisha kwa kuhakikisha kuwa watu wanapata madawa ya bei nafuu katika vituo vya afya vya umma na kwa wakati unaofaa.