Ubongo Learning
Interactive Infotainment for Economic Empowerment
Profile details
Likes:
Comments:
0
Mradi
Interactive Infotainment for Economic Empowerment
Kiongozi wa Timu
Shezheen Ladha
Timu
Nisha Ligon, Shezheen Ladha, Doreen Kessy, Anold Thadei, Christina Bwana and Cvetta Ngoma
Kuhusu sisi
Ikiwa kama taasisi ya mafunzo, tunataka kupanua maudhui yetu yanayoburudisha na kuelimish na na takwimu/data husika na uchumi ili kuboresha uwezeshaji wa kiuchumi kwa wasichana, na kuongeza usalama wao, na uwezo wa kujitegemea.
Mada
Kutanua Uwezeshaji wa Kiuchumi na mikakati ya kuongeza uchumi wa kujitegemea kwa wasichana na wanawake vijana.
Ufumbuzi
Ubongo Learning tayari ina uhusiano na wasikilizaji wa kaya milioni 2.1 (ikiwa ni pamoja na wasichana 900,000) kupitia njia zetu zilizopo. Tutaweza kuunganisha uhusiano huu kufikia wasichana kupitia mfumo wa burudisha-elimisha ambao utaboresha elimu yao ya kifedha. Kwa kuongeza uelewa juu ya takwimu/data kwa upande tukiwa tunajenga uelewa wa masuala ya fedha, tutawawezesha wasichana kutumia takwimu husika kuhusu elimu na uchumi katika kufanya maamuzi juu ya maisha yao. Kupitia mpango huu, tunatarajia kuboresha uwezeshaji wa kiuchumi wa wasichana na kuboresha usalama wao na uwezo wa kujitegemea. Baada ya muda, hii itaongeza mahitaji ya takwimu/data kwa kuipatia hadhira yetu takwimu juu ya elimu na uchumi, kujadiliana na kuwashawishi wazifanyie tathmini jinsi gani zinamahusiano na maisha yao. Tutatoa takwimu/data zetu na mrejesho kwa wadau muhimu na kushirikiana ili kuunda sera ambayo inaweza kuleta mabadiliko ya uwezeshaji wa kiuchumi kwa wasishana nchini Tanzania.
Categories: