Bw. Suleiman Hamyar Suleiman kwa sasa anafanya kazi SUZA (State University of Zanzibar kama mratibu wa miradi ya Mwaka wa mwisho katika Idara ya Sayansi na Teknolojia ya Habari, pia anafanya kama mwenyekiti wa TANIE (Tanzania information Ethics) na Zaidi ya yote ana uzoefu wa zaidi ya miaka kumi katika ufundishaji katika nyanja ya Teknolojia ya Habari yaani TEHAMA.
Bw. Suleiman pia ana Shahada ya Uzamili katika kubuni bidhaa za umeme aliyopata katika chuo cha Glarmorgan U.K (2003), Pia amehitimu Diploma ya juu katika kazi za jamii kutoka Open University of Tanzania (2013). Mr. Suleiman alipata Shahada yake ya kwanza ya Sayansi Ngamizi kutoka Mysore University India (2000). Pia amepata mafunzo mbali mbali katika Nyanja ya Ujasiriamali, Uvumbuzi, Ufundishaji na Usimamiaji.
Mr. Suleiman anapenda kujihusisha shughuli za Maadili ya katika Sekta ya Habari, Mitandao, Ukaguzi wa teknolojia ya habari, Kusimamia seva za Windows na Linux, kuwawezesha vijana kupitia ubunifu na uvumbuzi, na mambo mengine yanayo husiana na maendeleo ya jamii na Ujasiriamali.