Kama Meneja Uhamasishaji na Mshauri, Mwasiti anaratibu mipango yote ya DLIIC ya ushauri Kwa washindi wa shindano. Anawasaidia washauri na washauriwa katika kufikia malengo yao na kuratibu mafunzo ili kuwajengea washauriwa uwezo wa kiujuzi baada ya kufanyika tathmini.