Musafiri Mbilinyi
Jilinde Game
Profile details
Likes:
Comments:
0
Mradi
Jilinde Game
Kuhusu mimi
Nikiwa kama mhuishaji na mtengeneza michezo ya kompyuta, nataka kuleta muunganisho baina ya burudani na takwimu/data kwa kutumia nguvu ya michezo ya simu za mkononi katika kupiga vita VIRUSI vya UKIMWI/UKIMWI miongoni mwa wasichana na wanawake vijana. Mchezo wangu utawashawishi wasichana na wanawake vijana kufanya maamuzi sahihi katika maisha yao na kufikia malengo yao.
Mada
Kuongeza nafasi za uongozi na ufanyaji wa maamuzi kwa wasichana na wanawake vijana katika vita dhidi ya Virusi vya Ukimwi
Timu
Praygod Penieli, Joseph Mushi, and Wilfred Bahati
Ufumbuzi
Jilinde ni mchezo wa simu za mkononi ambapo mhusika mkuu ni mwanamke kijana ambaye ni lazima apambane na vizuizi vinavyomuongezea yeye nafasi ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Katika mlengo huo, pia anaweza kuchagua maeneo chanya ambayo yatasaidia katika kuboresha maisha yake. Mchezo umejuisha maswali ambayo yanamwezesha mchezaji kupata taarifa zaidi juu ya Virusi Vya Ukimwi/Ukimwi. Mchezo huu pia utawekwa kwenye tovuti pamoja na jukwaa ambalo wasichana na wanawake vijana watajadiliana juu ya changamoto zao za maisha.
Categories: