Mkata Nyoni
TanzMED
Profile details
Likes:
Comments:
0
Mradi
TanzMED
Kuhusu mimi
Nikiwa kama mbunifu, nataka nitumie TanziMED na takwimu/data ili kuongeza utoaji, utumiaji na upeanaji wa taarifa za kiafya ili kufikia malengo mbali mbali. Kukuza ushirikishwaji wa wanaume wenza katika utengenezaji wa mazingira salama kwa wasichana na wanawake vijana; kuwalinda wasichana na wanawake vijana dhidi ya hatari vya kuambukizwa VVU/Ukimwi na pamoja na magonjwa mengine ya STDs, na kutengeneza vyanzo mbalimbali vya mapato na ajira kwa wafanyakazi wa afya.
Mada
Kuongeza ushiriki wa wanaume katika utengenezaji wa mazingira salama kwa wasichana na wanawake vijana.
Timu
Lucy Johnbosco, Joseph Chuwa, Nauma Maarifa, Sophia Mangapi, Peter Mtavangu
Ufumbuzi
Urikishwaji wa wanaume umekuwa ni changamoto kubwa katika vita dhidi ya VVU. Hii ni sehemu tu, sababu kampeni nyingi zinashindwa kuwafikia wanaume wenza sababu ya masuala ya kibaguzi na majukumu ya kijamii. Pia, nchini Tanzania, kuna mifumo michache inayowawezesha watumiaji kupata elimu na ushauri kwa urahisi. Ingawa mifumo kama AfyaPal, AfyaCall na mingine inatoa elimu juu ya afya, hawamalizi mzunguko wa taarifa, kwa mfano, wanaweza mpatia mtu elimu lakini siyo ushauri wa wapi kwenda baada ya hapo. Pia, hakuna njia rahisi ya kupata ushauri mtandaoni toka kwa wataalam wa afya. Mwisho wake, hii mifumo inakuwa haijitoshereshi katika kutoa huduma kamilifu katika vita dhidi ya VVU/UKIMWI.Aidha, Watanzania wasichana 780,000 wenye umri zaidi ya miaka 15 hawana chanzo kamili cha kimtandao kujifunza juu ya jinsi gani ya kujilinda dhidi ya VVU/UKIMWI wakishaingia katika umri wa kubarehe. Ili kupigana na tatizo hili, tunahitaji kuwawezesha watanzania kupitia elimu ya afya na taarifa muhimu. Hususani tunatakiwa kuwafikia washirika wa kiume.TanzMED inatoa elimu ya kiafya ambayo itawaelimisha wanaume jinsi gani ya kuwalinda wasichana na wanawake vijana dhidi ya VVU/UKIMWI na umuhimu wa kufanya hivyo. TanzMED itakuwa na jukwaa la ushauri, ambalo linaweza kuwa la binafsi au Umma. Watumiaji wanaweza pata ushauri wakati wowote, mahali popote bila ya mtu mwingine kujua. Databezi za vituo vyetu zitawasaidia watumiaji kuweza kujua huduma ya afya iliyokaribu. Vituo hivi vinaweza kuwa Hospitali, Dispensari, Vituo Vya Arv, na vinginevyo. Tutaanzisha vilabu vya wanaume katika wilaya zitakazochaguliwa ili kuwapa ushawishi wanaume ushiriki katika kuwalinda wasichana na wanawake vijana kwa kutumia njia rafiki.
Categories: