MariaDorin Shayo
NIPO
Profile details
Likes:
Comments:
0
Mradi
NIPO
Kuhusu mimi
Timu yangu inataka kutumia App katika mfumo wa kompyuta kuweza kukusanya takwimu/data za utoro ili tupunguze kiwango cha uachaji shule, pamoja na hatari ya kupata maambukizi ya VIRUSI VYA UKIMWI na UKIMWI miongoni mwa wasichana na wanawake vijana.
Mada
Kupunguza uachaji shule wa mapema unaopunguza fursa kwa wasichana na wanawake vijana.
Timu
Bertha Sanga, Sherryen Mutoka, Baraka Cassian, Jacqueline, Catherine Kimaro
Ufumbuzi
NIPO ni App ya kompyuta inayosaidia kwenye ufuatiliaji wa maudhurio na kutuma ujumbe wa maramoja kwa wazazi juu ya utoro wa watoto wao usiokuwa na maelezo yoyote. Pamoja na kutuma taarifa, hii app pia inakusanya data za utoro na uachaji shule ambazo uweza kutumika kwa watunga sera katika kufanya maamuzi ya msingi. Utafiti umeonyesha kuwa asilimia 70 ya uachaji shule ni matokeo ya utoro uliokithiri. Kwa maana hiyo, tunaamini kuwa kwa kupunguza utoro, tutapunguza pia uachaji wa shule . Hivyo, tunaamini kuwa kwa kupunguza kiwango cha uachaji shule tutapunguza pia hatari ya wasichana na wanawake vijana kuambukizwa VIRUSI VYA UKIMWI/ UKIMWI sababu tafiti zimeonyesha kuwa kila mwaka msichana akikaa shule, upungukiwa na hatari ya kuambukizwa thelusi moja.
Categories: