Lulu Said Ameir
Be A Lady (Usimamizi wa Usafi wa Hedhi)
Maelezo ya wasifu
Likes:
Comments:
0
Project
Be A Lady (Usimamizi wa Usafi wa Hedhi)
About Me
Kama mjasiriamali mdogo, mimi nataka kufunga mashine za utengenezaji wa pedi kwenye mashule ili kuwasaidia wasichana waliobarehe kupata pedi safi na za bei nafuu. Lakini pia nataka kukusanya takwimu ili kupata uthibitisho wa jinsi gani mashine hizi zimeweza kupunguza utoro wa wasichana utokanao na hedhi. Lengo si kuwa tu mjasiriamali lakini pia niweze kufikia lengo langu la kuwasaidia wasichana wenzangu na wanawake, sababu ili tatizo kubwa tunalokumbana nalo kila siku.
Theme
Uwezeshaji kwa wananchi
Location
Dar es Salaam - Ilala Municipal Council, Kinondoni Municipal Council, Temeke Municipal Council
Team
Lulu Said Ameir, Dunia Said Nassoro, Kaijuko Jermaine Mukandala, na Elizabeth Samweli Mabelya
Solution
Ufumbuzi wangu ni ufungaji wa mashine za kutengeneza pedi katika maeneo kama vile Shule za Sekondari, na Vyuo vikuu ili kusambaza kwa watu wenye wa kipato cha chini pedi zenye ubora, na za gharama nafuu. Taarifa kutoka kwa matumizi ya mashine hizi zitatumika kulinganisha viwango vya mahudhurio ya shule na kufanya mapendekezo juu ya njia za kupunguza utoro mashuleni.
Scale up
Be A Lady tunatengeneza upya mashine za utoaji pedi ili kuongeza wingi wa bidhaa na pia kuboresha huduma kwa mtumiaji. Pia tunapanga kuweka mashine zetu kwenye shule nyingi zaidi ili kusaidia malengo ya serikali katika kusaidia wasichana wengi kushiriki kikamilifu katika elimu.
Categories: