TWENDE_Infographic
Justin Kashaigili
Twende
Profile details
Likes:
Comments:
0
Mradi
Twende
Kuhusu mimi
Justin Kashaigili ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Teknolojia ya Twende. Nikiwa kama mwanasayansi wa kompyuta mwenye ujuzi wa uhandisi wa mifumo ya kompyuta, uendeshaji na ujasiriamali, anataka kutumia teknolojia kuwaunganisha watu na usafiri ulio salama na wa uhakika, na hivyo kupunguza ajali za barabarani na uhalifu dhidi ya abiria. Na wakati huo huo, vijana madereva wataweza kutanua ukubwa wa wateja wao.
Mada
Kuendeleza na kukuza muunganiko baina ya vijana na fursa za kiuchumi
Timu
Gabriel Gabriel, Aron Katokololo
Ufumbuzi
Twende, ni mfumo wa simu unaosaidia kupata kwa urahisi dereva wa taxi, na bajaji ambao wanavigezo, wamethibitishwa, wa uhakika na salama. Mfumo unatumia teknolojia ya GPS kuweza kupata sehemu mtumiaji wa huduma alipo na kuandaa safari yake. Watumiaji pia wanaweza kutumia Twende kukodi gari na dereva kwa safari moja au zaidi.Mfumo wa Twende umejumuisha orodha ya madereva ambayo wamechagulia kulingana na rekodi zao za usalama barabarani na uhalifu, leseni halali ya udereva, pamoja na uthibitisho wa kusomea udereva kutoka katika chuo kilichothibitishwa. Kwa kuwaunganisha watumiaji na madereva, Twende inawalinda madereva dhidi ya ajali na wahalifu. Mfumo pia unatoa orodha ya makampuni yanayokodisha magari ambayo yanaweza kutoa magari kwa watumiaji wanaohitaji kuyakodi kwa siku moja au zaidi.
Categories: