Judith Leo
Early-warning Dropout Visualization (EDV) Tool
Profile details
Likes:
Comments:
0
Mradi
Early-warning Dropout Visualization (EDV) Tool
Kuhusu mimi
Nikiwa kama kijana mwanasayansi katika takwimu/data, tanaka kutumia takwimu/data zenye ubora wa juu kwenye kifaa ambacho kitasaidia kupunguza uachaji shule kwa wasichana na kwa upande mwinine kufikia malengo ya kupunguza maambukizi ya VIRUSI Vya UKIMWI kwa wanawake vijana.
Mada
Kupunguza uachaji shule wa mapema unaopunguza fursa kwa wasichana na wanawake vijana.
Timu
Prisila Ishabakaki, Sarah Nyanjara, Neema Mduma, Andrea-Michael Kileo, Himili Mbawala and Janeth Marwa
Ufumbuzi
Mradi huu utaangazia changamoto ya ukusanyaji wa data, utoaji wa data kwa wakati na utumiaji wa data kwa ufasaha kuanzia ngazi ya chini (Shule, Kijiji na Wilaya) mpaka ngazi za juu kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa. Kwa kutumia teknolojia zenye unafuu wa bei kwa ajili uwekaji wa takwimu kitaswira na kutumia simu, mradi utarahisisha utoaji wa takwimu, uchambuzi, na uwasilishaji kutoka ngazi moja mpaka nyingine. Kifaa cha EDV kitatumia teknolojia ya simu na taswira katika kutengeneza uwasilishaji unaoeleweka wa hali ya uachaji shule. Baada ya hapo, hali ya uachaji shule itatolewa kwa mtumiaji kupitia meseji kwenye simu ya mkononi, na kusaidia vyombo vya ngazi za chini kuchukua hatua haraka ili kuzuia suala la uachaji shule. Kifaa hiki kitapunguza viatarishi vya maambukizi ya VVU kwa kutambua wanafunzi wale waliopo katika mazingira hatarishi ya kuacha shule na kuchukua hatua maalum. Kifaa pia kitaongeza uwezo wa kutumia takwimu/data zilizo katika ubora wa hali ya juu.
Categories: