Hussein Juma Kiranga
Rate My School Application
Profile details
Likes:
Comments:
0
Mradi
Rate My School Application
Kuhusu mimi
Kwa mujibu wa ripoti ya elimu ya PO RALG, kiwango cha uachaji shule kimefikia asilimia 10 kadirio. Nataka nitumie jukwaa la mtandao kuweza kutengeneza takwimu/data juu ya maudhurio ya wanafunzi ili kuweza kuboresha ufuatiliaji na kuchukua hatua stahiki ili kupunguza uachaji wa shule.
Mada
Kupunguza uachaji shule wa mapema unaopunguza fursa kwa wasichana na wanawake vijana.
Timu
Gwaliwa Mashaka, Revocatus Lembeli, Neema S. Chande
Ufumbuzi
Tunautambulisha mfumo wetu wa kimtandao unaoitwa Rate My School ambao utatoa takwimu/data juu ya maudhurio ya wanafunzi na matokeo yao ya shule. Jukwaa ili pia litatoa nafasi ya kupeana taarifa juu ya mazingira ya shule (Ubora wa majengo, vyoo, uwiano wa wanafunzi na walimu na zaidi). Wazo si kutoa taarifa pekee lakini pia kushawishi watekelezaji mbali mbali (Washauri, Wabunge, Bodi za Shule, na Uongozi wa Shule, Taasisi za Kitafiti, Walimu, Wazazi na jamii kwa ujumla) kuchukua hatua stahiki katika kushughulikia tatizo la uachaji shule. Ushirikishwaji wa jamii hautapunguza uachaji shule kwa wasichana pekee lakini hata kupunguza mimba isiyotarajiwa na kushusha hatari ya maambukizi ya VVU.
Categories: