George Elly Matto
AfyaBox
Maelezo ya wasifu
Likes:
Comments:
0
Project
AfyaBox
About Me
Kama mtafiti ambaye nataka kusaidia jamii yangu, nataka kutumia teknolojia ya simu ili kuwezesha upatikana wa taarifa sahihi kutoka kwa Msajili wa Kituo cha Afya na kuhakikisha zinapatikana kupitia simu zote za mkononi kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili ili kila mtu aweze kupata taarifa za vituo vya afya nchini Tanzania.
Theme
Upatikanaji wa huduma bora za afya na taarifa
Location
Moshi
Team
George Elly Matto, Makwani John Chimagu, Pascal Thadeus Msoka, na Thadei Mlkiory Msumanje
Solution
Mfumo utokanao na simu za mkononi ambao unalenga kuongeza matumizi ya Mfumo wa Usajili wa Kituo cha Afya (HFR) - na kuwezesha upatikanaji wa wa taarifa zilizoidhinishwa kuhusu vituo vyote vya afya Tanzania Bara. Mfumo huo wa simu utatokana na teknolojia ya USSD unaopatikana kupitia kila aina ya simu za mkononi na utapatikana kwa lugha zote Kiswahili na Kiingereza.
Scale up
Tunataka kutanua upatikanaji wa afyaBox kwa Tanzania mzima, tukianzia katika mikoa yote Kilimanjaro na Arusha. Pia tuna mpango wa kuongeza vitu na huduma ambazo ziliombwa na Wizara ya Afya na TAMISEMI ili kuwaunganisha na vituo vya afya. Hususani, afyaBox itatoa huduma ya usafiri pale utakapohitajika kulingana na eneo la kituo cha afya. Pamoja na ilo, watumiaji watapewa nafasi kuchagua aina gani ya usafiri wanayohitaji. Kipengele cha pili kitakachoongezwa kitakuwa uwekaji wa mihadi na dokta kabla hujatembelea kituo cha afya. Kipengele kingine kitamwezesha mgonjwa kutoa mrejesho kwa dokta au mtu aliyemuhudumia.
Categories: