Eunice Likotiko
Genge Mkononi
Profile details
Likes:
Comments:
0
Mradi
Genge Mkononi
Kuhusu mimi
Nikiwa kama mwanamke kijana anaeamini katika uwezo wa teknolojia wa kushawishi na kuwezesha watu kubadirisha maisha yao, nataka kutumia teknolojia ili kuwasaidia vijana wanaojihusisha katika uuzaji wa bidhaa za kilimo kwa kuwapatia App itakayowaunganisha na wanunuzi na kuwapatia takwimu za uendaji wa soko na kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kibiashara.
Mada
Kuendeleza na kukuza muunganiko baina ya vijana na fursa za kiuchumi.
Timu
Eunice David Likotiko, Joyce Philipo Mnunguli, Winifrida David Likotiko
Ufumbuzi
Vijana wengi wa kitanzania wanafanyakazi katika sekta ya kilimo, wakiuza mazao kama vile, mbogamboga, matunda, nafaka na bidhaa zitokanazo na maziwa. Vijana hawa, wafanyabiashara wadogo watakutana na changamoto kama vile kuwa na wateja wachache, kutokuwa na hatua bira za uuzaji, mabadiriko ya bei na utaratibu mbovu wa utunzaji kumbukumbu. Genge Mkononi inatoa mfumo wa suluhisho linalotumia simu ya mkononi ambayo linawaunganisha wauzaji wa mazao ya chakula na wateja wao, na kuwezesha uuzaji wa bidhaa zao kupitia simu. Genge Mkononi itatumia takwimu zitakazo zalishwa kupitia app hiyo ili kuchakata mwenendo wa mauzo na kubashiri ni bidhaa gani zitahitajika zaidi katika siku za usoni, na ni wapi bidhaa hizi zitahitajika zaidi. Tatuzi hii itawasaidia wafayabishara wadogo kutanua wingi wa wateja wao, kuboresha uwezo wao wa utunzaji wa kumbukumbu za mauzo na kuandaa bidhaa zao kulingana na mahitaji halisi. Na hatimaye, huduma hii itaboresha vipato vyao na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Categories: