Denis Minja
Maasai Mart
Profile details
Likes:
Comments:
0
Mradi
Maasai Mart (Jukwaa la masoko ya kimtandao kwa bidhaa na utalii wa ndani na huduma)
Timu
Dina Zawadi Machuve, Salimu Yusufu Salimu, Kelvin Ngunjiri Kuria, Juma Bakari Muya, Leonia Baltazari Mluge, Elizabeth Juma Said
Kuhusu sisi
Kama timu ya wataalamu wa teknolojia na wataalam wa biashara mtandaoni, tunataka kuunganisha takwimu na teknolojia ya biashara mtandaoni pamoja na teknolojia ya simu ili kuunda jukwaa la biashara ya mtandaoni ya bidhaa za utalii na huduma, ili wauzaji wa ndani waweze kupanua mapato yao zaidi ya soko la ndani na ununuzi wa papo kwa papo kwa kuweza kupata masoko ya nje ya mipaka na ya kimataifa.
Mada
Kuendeleza na kuhamasisha muunganisho kati ya vijana na fursa za kiuchumi
Ufumbuzi
Maasai Mart inaruhusu wauzaji wa ndani na makampuni ya utalii kutangaza bidhaa na huduma zao kwenye soko la mtandaoni, na hivyo kuongeza fursa kwa vijana wenye vibanda vya biashara na kuwezesha vijana ambao hawana uwezo wa kuanzisha biashara ya wazi. Jukwaa litawezesha yafuatayo: kutengeneza wa wasifu wa mtandaoni kwa wachuuzi wa ndani na makampuni ya utalii; Ununuzi wa bidhaa mtandaoni na huduma; Orodha ya bidhaa na huduma mtandaoni; Uwepo wa Ishara za wakati za ofa na mapunguzo; mauzo ya mtandaoni; kufuatilia mwenendo wa bidhaa na huduma. Kwa kutumia Maasai Mart, wachuuzi wa ndani wanaweza kufikia masoko nje mipaka na ya kimataifa na bidhaa na huduma zao, badala ya kutegemea tu ununuzi wa ndani na wa uso kwa uso.
Categories: