Dainess William Mngazija
MegaFin
Profile details
Likes:
Comments:
0
Mradi
MegaFin (Kuhifadhi rekodi za kifedha na jukwaa la elimu)
Kuhusu mimi
Mimi ni mhitimu wa teknolojia ya habari sasa nafanya kazi katika sekta ya kifedha kama afisa wa mkopo katika taasisi ya fedha inayolenga wanawake wenye kipato cha chini jijini Dar es Salaam. Kama mwanamke na mwanateknolojia, nataka kutumia takwimu ya idadi ya watu, fedha na bima ili kuwawezesha wanawake na vijana na dhana za usimamizi wa kifedha na elimu kwa lengo la kuboresha masuala yao ya kifedha.
Mada
Kukuza uwezo wa kiuchumi wa vijana
Timu
Dainess William Mngazija, Abas Majid Ismail, Angel Robert Nsanya, Dickson Nganga Gikuni
Ufumbuzi
MegaFin ni huduma ya maendeleo ya kifedha ambayo uwawezesha wale wasiofikiwa na huduma za kifedha na benki kufikiwa na elimu ya fedha, zana za usimamizi, na mbinu za kiuwekezaji. Jukwaa hutoa upatikanaji wa mtandao wa elimu ya kifedha, taarifa za masuala ya fedha, michango midogo midogo, akiba ndogo ndogo, na bima ndogo. MegaFin huwapa watumiaji njia rahisi ya kusimamia kumbukumbu za fedha, ambayo inawawezesha kujua hali zao za kifedha na upatikanaji wa fedha. Huduma pia inaunganisha watumiaji na bima, akiba, na watoa taarifa. Lengo letu ni kuwawezesha vijana na wanawake kufikia lengo la kuwa na huduma za kifedha jumuishi na uhuru.
Categories: