Bukhary Haruna Kibonajoro
OKOA
Maelezo ya wasifu
Likes:
Comments:
0
Project
OKOA
About Me
Kama mbunifu mdogo na mjasiriamali katika sekta ya teknohama, nataka kutumia takwimu zenye ubora za huduma ya afya ili kutoa urahisi katika upatikanaji wa huduma bora za afya - hasa upatikanaji wa madawa kwa watu masikini ambao kwa kawaida hutafuta huduma katika vituo vya afya ili tuweze KUWAOKOA: Katika kuokoa muda, kuokoa pesa, kuokoa maisha kwa kuhakikisha kuwa watu wanapata madawa ya bei nafuu katika vituo vya afya vya umma na kwa wakati unaofaa.
Theme
Upatikanaji wa huduma bora za afya na taarifa
Location
Kigoma Ujiji
Team
Bukhary Haruna Kibonajoro, Muslim Haruna Kibonajoro, Haji Issa Rubibi, na Selemani Haruna Kibonajoro
Solution
Programu ambayo inaweza kufuatilia madawa na vifaa vya matibabu kwa wakati halisi kutoka MSD hadi katika hospitali, zahanati hadi vituo vingine vya afya, na inaweza kutumika wakati huo huo na Vituo vya Afya, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wizara ya Afya, Idara ya Matibabu ya Tanzania (MSD, Kikanda/ Kitaifa) na wananchi katika eneo fulani. Mfumo huu unajaribiwa katika manispaa mbili na unahitaji kukuzwa zaidi.
Scale up
OKOA imetekelezwa katika vituo vyote vya afya katika Manispaa ya Kigoma Ujiji. Katika mwezi mmoja, tovuti ilipokea watu 2,264 ambao waliitembelea kuangalia upatikanaji wa madawa hali ya msongamano wa watu katika vituo vya afya. Sasa, OKOA inajitanua zaidi kufikia vituo vya afya 34 katika Wilaya ya Kyela na kuongeza huduma ya USSD ili kuwafikia watumiaji wenye kipato cha chini, ambao hawawezi kufikiwa na huduma ya intaneti. Timu yetu pia inategemea kuioanisha OKOA na mifumo mingine ya afya kama vile Got-HOMIS, Epicor 9 na ELMS kwa ajili ya upatikanaji wa takwimu na ufanyaji wa maamuzi.
Categories: