Mr. Ahmada Lyamaiga amekuwa mfanyakazi wa kitengo cha teknolojia ya habari tangu mwaka 1973. Alihitimu katika chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka 1978 na shahada ya uzamili ya sayansi ya kompyuta na kuhudhuria kozi mbalimbali za muda mfupi ndani na nje ya nchi, akisomea utaratibu wa kompyuta, mfumo uchambuzi wa kipekee, mitandao ya kompyuta na masimulizi. Ameandika taratibu za komputa kwa Java, Visual Basic, Cobol, Fortran, XML na Pascal.
Mr. Lyamaiga ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaaji wa Ports and Maritimes Consultancy Services Company Limited, iliyoanzishwa mnamo mwezi wa nne mwaka 2008. Kampuni inajihusisha na utengenezaji wa programu tumizi, masoko na usambazaji. Pia ni kiongozi wa utengenezaji wa program tumizi katika mfumo wa usimamizi SACCOS. Katika kitengo hichi amedhamilia kusaidia wanachama wa SACCOS kwa kuboresha uendeshaji wao kuwa wa kisasa na wa gharama nafuu.
Kwa kutengeneza historia ndefu katika ubobezi wa teknolojia ya habari kwa miaka kumi iliyopita Mr. Lyamaiga ameongoza timu ya utengenezaji wa vifurushi vya kompyuta na kutoa huduma za ushauri katika vitengo vya uhasibu, usindikaji mishahara, usimamizi wa mfumo wa habari michakato ya mfumo wa biashara na kupitishwa kwa teknolojia ya habari katika taratibu za biashara.
Kabla ya kustaafu kutoka utumishi wa umma mnamo mwezi wa tisa mwaka 2008, Mr. Lyamaiga alikua msimamizi wa kurugenzi ya usimamizi huduma, ambayo inajumuisha huduma za teknolojia ya habari za TPA ambazo ni tofauti ila zenye ufanano, kazi za kuimarisha utendaji na kukuza mtiririko wa habari, kufuata na kuweka jumla ya kiwango cha ubora, huduma za maktaba na tathmini ya kazi. Usimamizi wa shughuli hizi, pamoja na usimamizi wa mafunzo, uliimarisha usimamizi wa ujuzi na mawasiliano ya Mr. Lyamaiga kwa wakati huo.
Mr. Lyamaiga pia alifanya kazi kama mkurugenzi wa huduma za usimamizi TPA/THA; msimamizi wa idara ya nguvu kazi ya wafanyakazi 52. Yeye mwenyewe aliongoza utekelezaji wa jumla ya ushirikiano wa mfumo wa kompyuta katika shughuli zote za bandari, ikijumulisha kazi za baharini na bandarini na hifadhi ya ofisi.
Zaidi ya kazi hii, Mr. Lyamaiga amefanya kazi kama mshauri juu ya miradi ya kimataifa. Hizi kazi zilijumuisha mratibu mkuu wa kuunda jumuiya ya bandari na maendeleo ya jukwaa la kawaida la kubadilishana habari za meli na mizigo kati ya wadau; mwenyekiti wa barabara za usafiri afrika mashariki kamati ya ufundi inayohusishwa kushirikiana habari juu ya harakati za kuagiza au kusafirisha mizigo katika barabara za kaskazini na kati; na mwanachama wa timu ya utekelezaji wa mfumo wa habari wa mizigo ulioendelezwa na UNCTAD ili kuwezesha usafirishaji wa biashara kwa nchi wanachama wa COMESA.