Profile Category: 3rd Challenge Winner

Ability Kakama
Profiles

Ability Kakama

Mimi ni mchumi, na Mchambuzi wa Biashara, nikiwa na lengo la kutanua fursa za kiuchumi kwa vijana, nataka nitumie data/takwimu na teknolojia ya kidijitali kurahisisha ujumuishi mpana wa vijana katika kazi za uzalishaji, na fursa nzuri za kiuchumi.

Eunice Likotiko
Profiles

Eunice Likotiko

Nikiwa kama mwanamke kijana anaeamini katika uwezo wa teknolojia wa kushawishi na kuwezesha watu kubadirisha maisha yao, nataka kutumia teknolojia ili kuwasaidia vijana wanaojihusisha katika uuzaji wa bidhaa za kilimo kwa kuwapatia App itakayowaunganisha na wanunuzi na kuwapatia takwimu za uendaji wa soko na kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kibiashara.

Denis Minja
Profiles

Denis Minja

Kama timu ya wataalamu wa teknolojia na wataalam wa biashara mtandaoni, tunataka kuunganisha takwimu na teknolojia ya biashara mtandaoni pamoja na teknolojia ya simu ili kuunda jukwaa la biashara ya mtandaoni ya bidhaa za utalii na huduma, ili wauzaji wa ndani waweze kupanua mapato yao zaidi ya soko la ndani na ununuzi wa papo kwa papo kwa kuweza kupata masoko ya nje ya mipaka na ya kimataifa.

Twende Social Innovation Center
Profiles

Twende Social Innovation Center

Kama kituo cha ubunifu wa kijamii, Twende huwezesha watu kubuni na kufanya teknolojia zinazoweza kutatua changamoto za jamii. Tunataka kuandaa na kuzitoa data kuhusu nani anayefanya teknolojia gani, kwa hivyo watumiaji wa ndani wanaweza kuungana na wabunifu wengine wa ndani, na soko la teknolojia inayofaa linaweza kuanzishwa nchini Tanzania.

Ekihya Limited
Profiles

Ekihya Limited

Kama mtoa suluhisho la mwisho kwa mwisho kwa waajiri kwenye soko, tunatarajia kutumia data na akili ya bandia (AI) kusaidia kutambua na kukuza talanta ili tuweze kuwawezesha vijana kupata kazi.

Reuben Mbwiga
Profiles

Reuben Mbwiga

Kama nikiwa kiongozi mdogo lakini mwenye uzoefu katika sekta ya huduma za kibenki na fedha, nataka kutumia ujuzi wangu, uhusiano na uzoefu wangu kukusanya data za ajira na kuzalisha ujuzi wa kuajiriwa kuandaa kikundi cha pili cha viongozi wadogo ili tuweze kuongeza uajiri wa vijana nchini Tanzania.

Gwaliwa Peter Mashaka
Profiles

Gwaliwa Peter Mashaka

Kama mtaalamu wa takwimu/data na teknolojia nataka kutumia teknolojia na data kuongeza upatikanaji wa ajira bora kwa watu wenye ulemavu kwa kutatua changamoto wanazokabiliana nazo wakati wa kutafuta au kuanzisha kazi.

Kakute Project
Profiles

Kakute Project

Ikiwa kama Taasisi ya Kibiashara ya Kijamii, tunatengeneza mtandao wa vijana waliopo vijijini Tanzania nzima, kwa kuunganisha taasisi zinazoongozwa na vijana na takwimu/data wanazohitaji kwa ajili ya kufanya maamuzi katika utoaji wa bidhaa zao na huduma.

Dainess William Mngazija
Profiles

Dainess William Mngazija

Mimi ni mhitimu wa teknolojia ya habari sasa nafanya kazi katika sekta ya kifedha kama afisa wa mkopo katika taasisi ya fedha inayolenga wanawake wenye kipato cha chini jijini Dar es Salaam. Kama mwanamke na mwanateknolojia, nataka kutumia takwimu ya idadi ya watu, fedha na bima ili kuwawezesha wanawake na vijana na dhana za usimamizi wa kifedha na elimu kwa lengo la kuboresha masuala yao ya kifedha.

Justin Kashaigili
Profiles

Justin Kashaigili

Nikiwa kama mwanasayansi wa kompyuta mwenye ujuzi wa uhandisi wa mifumo ya kompyuta, uendeshaji na ujasiriamali, anataka kutumia teknolojia kuwaunganisha watu na usafiri ulio salama na wa uhakika, na hivyo kupunguza ajali za barabarani na uhalifu dhidi ya abiria. Na wakati huo huo, vijana madereva wataweza kutanua ukubwa wa wateja wao.