Nikiwa kama Afisa Rasilimali Watu Upande wa Afya, nataka kutumia tawimu/data dhidi ya unyanyasaji kwa wasichana na wanawake vijana, ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya – hususani zile zinazohusiana na VVU/UKIMWI na kuchangia katika upunguzaji wa VVU/UKIMWI kwa ujumla.
Profile Category: 2nd Challenge Winner
Leyla Hamis Liana
Kwa mujibu wa USAID, wasichana 17,000 upata maambukizi mapya ya VVU kila mwaka na mbinu za ufundishaji za sasa hazitosherezi. Timu yetu itatumia michezo ili kuwaelimisha wanaume wenza, kuanzia miaka ya 15-24 na kuzalisha takwimu/data juu ya mienendo yao.
Hussein Juma Kiranga
Kwa mujibu wa ripoti ya elimu ya PO RALG, kiwango cha uachaji shule kimefikia asilimia 10 kadirio. Nataka nitumie jukwaa la mtandao kuweza kutengeneza takwimu/data juu ya maudhurio ya wanafunzi ili kuweza kuboresha ufuatiliaji na kuchukua hatua stahiki ili kupunguza uachaji wa shule.
Mkata Nyoni
Nikiwa kama mbunifu, nataka nitumie TanziMED na takwimu/data ili kuongeza utoaji, utumiaji na upeanaji wa taarifa za kiafya ili kufikia malengo mbali mbali. Kukuza ushirikishwaji wa wanaume wenza katika utengenezaji wa mazingira salama kwa wasichana na wanawake vijana; kuwalinda wasichana na wanawake vijana dhidi ya hatari vya kuambukizwa VVU/Ukimwi na pamoja na magonjwa mengine ya STDs, na kutengeneza vyanzo mbalimbali vya mapato na ajira kwa wafanyakazi wa afya.
Judith Leo
Nikiwa kama kijana mwanasayansi katika takwimu/data, tanaka kutumia takwimu/data zenye ubora wa juu kwenye kifaa ambacho kitasaidia kupunguza uachaji shule kwa wasichana na kwa upande mwinine kufikia malengo ya kupunguza maambukizi ya VIRUSI Vya UKIMWI kwa wanawake vijana.
Fatma Abbas Kombo
Nikiwwa kama mwanamke kijana, nataka nitumie mfumo wa kimtandao kuwaunganisha vijana na taarifa pia kuwapa ushauri wa elimu ya kujamiiana na hatari ya kuambukizwa VIRUSI vya UKIMWI, tukiwa tunaangazia vituo vya kupimia VIRUSI Vya UKIMWI, kuhakikisha kuwa wasichana na wanawake vijana wana taarifa iliyokamilika ambayo inaweza kuwalinda dhidi ya VIRUSI Vya Ukimwi.
Ubongo Learning
Ikiwa kama taasisi ya mafunzo, tunataka kupanua maudhui yetu yanayoburudisha na kuelimish na na takwimu/data husika na uchumi ili kuboresha uwezeshaji wa kiuchumi kwa wasichana, na kuongeza usalama wao, na uwezo wa kujitegemea.
Musafiri Mbilinyi
Nikiwa kama mhuishaji na mtengeneza michezo ya kompyuta, nataka kuleta muunganisho baina ya burudani na takwimu/data kwa kutumia nguvu ya michezo ya simu za mkononi katika kupiga vita VIRUSI vya UKIMWI/UKIMWI miongoni mwa wasichana na wanawake vijana. Mchezo wangu utawashawishi wasichana na wanawake vijana kufanya maamuzi sahihi katika maisha yao na kufikia malengo yao.
MariaDorin Shayo
Timu yangu inataka kutumia App katika mfumo wa kompyuta kuweza kukusanya takwimu/data za utoro ili tupunguze kiwango cha uachaji shule, pamoja na hatari ya kupata maambukizi ya VIRUSI VYA UKIMWI na UKIMWI miongoni mwa wasichana na wanawake vijana.
Wilson Mnyabwilo
Mimi ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bwilotech Co. Ltd. Nitafahamu maumivu ya kuacha shule, kwa hivyo ninatengeneza vitu vya kibunifu ili kuwalinda wanafunzi wasipatwe athari ya kuacha shule. Nikiwa kama mtengenezaji wa program za kompyuta na kijana mjasiriamali, nataka nitumie vyote teknolojia ya data na teknolojia ya habari ili kuwezesha ushirikishwaji wa wazazi katika suala zima la elimu la watoto wao. Lengo langu ni kupunguza utoro na kiwango cha uachaji shule kwa wasichana na wanawake vijana.