KUHUSU SISI
DHAMIRA YETU
Sisi tunawalenga Watanzania ambao ni wabunifu, wajasiriamali, na vijana ili waweze kutumia takwimu/taarifa na teknolojia katika kushughulikia matatizo magumu ambayo yanaiathiri nchi na jamii.
MALENGO YETU
DLI Innovation Challenge ina lengo la kushirikisha, kusaidia na kuwaunganisha watanzania wabunifu,watengenezaji, watoa ufumbuzi kwa kila mmoja nchini Tanzania na kutoa nafasi za kuleta mabadiliko katika maisha ya watu kwa kuongeza matumizi au upatikanaji wa data/takwimu.
KARIBUNI
WABUNIFU WAKITANZANIA NA WAJASIRIAMALI!
Tunahitaji msaada wako ili kuonesha jinsi takwimu/taarifa na matumizi yake vinayoweza kufanya mabadiliko katika maisha ya watu! Je, wewe una nia ya kujiunga nasi?.
Kupitia mpango wa Data for Local Impact (DLI) Innovation Challenge ambao unatoa ruzuku kwa Watanzania (watu binafsi, vikundi na mashirika) ambao wana mawazo ya ubunifu kuhusu jinsi ya kutumia au kuchanganya takwimu/taarifa kwa njia mpya itakayowawezesha kupata ufahamu au kuwawezesha kwa kupitia huduma hiyo kubadilisha maisha yao kwa kubadilishana taarifa. Mbali na hilo, pia DLI Innovation Challenge ina lengo la kushirikisha, kusaidia na kuwaunganisha Watanzania ambao ni wabunifu, watengenezaji, na watoa ufumbuzi na kila mmoja mwenye nafasi ya kuleta mabadiliko katika maisha ya watu.
DLI Innovation Challenge inasaidia pia katika Malengo ya Maendeleo endelevu na katika maeneo ya maendeleo ya Afya na Ustawi (SDG 3), Usawa wa Jinsia (SDG 5), na mazingira bora ya kazi na Kukuza Uchumi (SDG 8).
DLI Innovation Challenge vilevile inatoa ruzuku kwa wabunifu wa ndani na inatafuta ufumbuzi bora kwa njia ya ushindani wa changamoto mpaka tano.
Dirisha la kwanza la shindano lilizinduliwa Oktoba 2016, na washindi wakatangazwa Machi 2017 na dirisha la pili linatarajiwa kufunguliwa Mei 2017. Kila shindano litajumuisha mada kuu tatu hadi tano.
Timu ya DLI Innovation Challenge itaandaa mada hizo kuu kwa kushirikiana na kushauriana na wadau husika mbali mbali nchini Tanzania. Mada hizo zitalenga zaidi kwenye masuala yaliyojitokeza katika dirisha lililopita na mafundisho yake na kujumuisha vipaumbele kutoka katika programu ya DCLI.
Wakati wa kila dirisha DLI Innovation Challenge itakuwa ikitoa msaada wa ruzuku ndogo katika madirisha yote mawili ambao ni kuanzia dola za Marekani 25,000 kila moja) na ruzuku kubwa hadi dola za Marekani 100,000 kila moja kwa watu binafsi na mashirika ya kitanzania kulingana na vigezo maalum.
Katika kila dirisha tunatarajia kutoa ruzuku 12 zitakazoanzia dola za kimarekani 10,000 mpaka 25,000 kila mmoja, pamoja na ruzuku mbili zitakazoanzia dola za kimarekani 75,000 mpaka 100,000. Kupitia mpango huo DLI Innovation Challenge itashirikiana na asasi za kuendeleza mawazo katika ufumbuzi ambazo zitakwenda sambamba na hilo. Wafumbuzi hao wataweza kuratibu maombi au dhana ambazo zinaweza kutatua tatizo husika katika kila pendekezo. DLI inatoa nafasi hiyo kwa Watanzania pekee wakiwa kama watu binafsi, vikundi au mashirika yaliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria.
TIMU YETU
Meneja Ruzuku
Collin Gumbu
Meneja wa Fedha
Nguza Kinonda
Afisa Ruzuku
Lazaro Kapaya
Meneja Uhamasishaji na Mshauri
Mwasiti Mkembe
Wafadhili
TAASISI ya Mpango wa Dharura wa Rais katika Mapambano dhidi ya UKIMWI (PEPFAR) na wa kukabiliana na Changamoto za Milenia (MCC) zimeshirikiana kwa kuwekeza dola za Marekani milioni 21.8 katika mpango wa Data Collaboratives for Local Impact (DCLI) katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa ajili ya mapambano dhidi ya VVU / UKIMWI, afya duniani, usawa wa kijinsia, ukuaji wa uchumi na kuboresha mipango, sera na maamuzi kwa wadau wote.
Mpango huo wa DCLI umeelekeza nguvu pia katika uboreshaji wa mfumo mzima wa takwimu/taarifa,ikiwa ni pamoja na matumizi ya hizo takwimu/taarifa katika ngazi za kikanda, na kuzidi kujenda mfumo wa namna ya kuchochea uwezo mkubwa wa kutumia takwimu/taarifa hizo kupitia mifumo ya ndani ya nchi.
DCLI inashirikiana na Serikali ya Marekani ili kuongeza ufanisi wa Idara ya utoaji misaada ya nje na kuongeza pia ushirikiano kimataifa ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu. (SDGs ). Soma zaidi…….
Washirika wetu
Dar es Salaam Teknohama Business Incubator (DTBi) wanashirikiana na Palladium kuiwezesha DLI Innovation Challenge, kutoa msaada wa kiufundi katika mchakato wa kuwapata washindi kwa njia ya mtandao na kuwasaidia wabunifu wakitanzania , watengenezaji na Watumiaji wa Takwimu.
Washirika