Mawasiliano

Dar es Salaam, TZ

info@dli.teknohama.or.tz

@DLIInnovation

Wasiliana Nasi

Maswali

Tuna mpango wa kufungua dirisha la pili la shindano ifikapo Mei 2017. Endelea kutembelea hapa upate taarifa juu ya mada kuu na ratiba. Ni lini dirisha la pili la shindano kufunguliwa?

Wote! Aidha hii ni mara yako ya kwanza kusikia kuhusu shindano la Ubunifu la DLI au umeweza kufika mpaka hatua ya mwisho katika shindano la kwanza, tunakuhitaji uchangie mawazo yako ya kibunifu kwa ajili ya kukuza matumizi ya takwimu yaani data nchini Tanzania.

DLI Innovation Challenge hufadhiliwa na PEPFAR kupitia mpango wa MCC-PEPFAR DCLI na unalenga katika jitihada zinazohusiana na Afya na Ustawi (SDG 3), Usawa wa Jinsia (SDG 5), na Kazi Bora na Ukuaji wa Uchumi (SDG 8). Kabla ya kila dirisha la shindano, DTBi inatumia mchakato shirikishi na ushirikiano na wadau wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya serikali husika na taasisi nyingine zinazohusiana na eneo husika la shindano. Orodha ndefu ya mada kuu hupitiwa, kurekebishwa, kuendelezwa na kupimwa wataalam husika kabla ya kuchagua mada kuu za mwisho za shindano.

Wale wabunifu! Tunayakubali mawazo mapya kwa ajili ya mchakato, mifumo, vifaa vya kimtandao. Pia tunakubali maombi yanayolenga kusaidia kukuza uvumbuzi/mradi. Angalia vigezo vya tathmini ili kuona kama wazo lako linaweza kuibuka mshindi. Mawazo yanapaswa kulandana na mada kuu za shindano aidha kukuza mahitaji ya takwimu zilizo bora au uwezo wa kutumia takwimu katika kuboresha maisha ya watanzania.