Tuma Maombi

Je upo tayari kwa shindano?

Pakua Kitabu cha Maelekezo kwa Muombaji, badilisha mawazo yako kuwa ufumbuzi, malizia maombi yako kupitia mtandao, na ushinde uweze kulitekeleza wazo lako!

Pakua Kitabu cha Maelekezo kwa Muombaji

Dirisha la kutuma maombi limefungwa. Endelea kutembelea ukurasa huu kwa habari zaidi.

Mada Kuu

Katika Dirisha hili la Shindano, DLIIC inashirikiana na World Food Programme (WFP), shirika linaloongoza duniani katika kupambana na njaa na utapiamlo. Dirisha hili linajulikana kama “Zero Hunger, Zero AIDS”, litalenga katika kuhakikisha kizazi kijacho cha watanzania kinakuwa kizazi chenye afya bora kupitia upatikanaji wa chakula cha kutosha, salama na chenye lishe. Mada kuu za shindano zipo hapa chini. Kwa maelezo zaidi juu ya mada kuu, tafadhali fungua na usome Jarida la Muombaji.

  1. Lishe, upatikanaji rahisi, nafuu na vyakula vizuri na vyenye bora
  2. Kumsaidia mkulima mdogo aliyethubutu

Vyanzo Vya Data

Tafuta vyanzo vya ziada vya data kutoka WFP.

Je Shindano la Ubunifu la DLI linatoa nini kwa washindi?

Washindi wa DLI Innovation Challenge watapata ruzuku ili kuwawezesha kuendeleza ufumbuzi uliopendekezwa kwa kipindi cha miezi 3-6. Mbali na kupata misaada ya kifedha, washindi watapewa mshauri ambaye atawasaidia kuendeleza mawazo yao ya ubunifu na kuwa kamili. Washindi pia watapata mafunzo na msaada wa usimamizi wa ruzuku kutoka kwa timu ya DLI.

Vigezo Vinavyohitajika – Je una vigezo?

Vigezo vya Tathmini