Wabunifu Tisa Wajishindia ruzuku kutoka Dirisha la Nne la Shindano la DLI

Wabunifu Tisa Wajishindia ruzuku kutoka Dirisha la Nne la Shindano la DLI

Shindano la Ubunifu la Data for Local Impact Innovation Challenge (DLIIC) limewachagua wabunifu 9 ikiwa ni Taasisi 5 na Watu Binafsi 4 kupokea ruzuku chini ya Dirisha la Nne la DLI. Dirisha hilo lililenga zaidi changamoto zilizopo katika jamii zilizotambuliwa na wananchi wa kawaida kupitia mradi dada wa Data Zetu ambao umelenga katika kukuza matumizi ya data katika ngazi ya chini. Changamoto hizo zilizotambuliwa na wananchi zilikuwa katika makundi makuu manne:

  • Mimba za utotoni
  • Unyanyasaji wa kimwili/Kijinsia
  • Matumizi ya madawa kulevya
  • Maendeleo ya Mtoto

Changamoto hizi ni zinazojulikana kwa jamii nyingi za kitanzania, na zinaweza kutatuliwa kupitia ubunifu utokanao na data, na kuendana na vipaumbele vya PEPFAR katika kupunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI.

Dirisha hili la nne la shindano lilifunguliwa mnamo Aprili 27 na kufungwa mnamo Juni 27, 2018. Jopo la wataalam majaji walichagua washiriki 41 ambao walitetea mapendekezo yao mubashara. Tisa kati ya hawa washiriki walichaguliwa kupokea ruzuku za DLIIC. Watu binafsi na timu ndogo ndogo zinapokea ruzuku kuanzia Dola za Kimarekani 10,000- 25,000, wakati Taasisi zinapokea kuanzia Dola 75,000-100,000. Ruzuku hii inatolewa pamoja msaada wa kitaalam kutoka katika timu ya DLI. Kutokana na kwamba mradi wa DLI unaelekea kufungwa ifikapo mwisho wa mwaka huu, washindi wa dirisha la nne watapokea ruzuku zao na msaada wa kitaalam kupitia Tanzania Data Lab (dLab) ambayo itaendeleza kazi za DLI katika miaka ijayo.

Akitoa maoni yake juu ya matokeo ya shindano hilo, Bw. Agapiti Manday, Meneja Mradi wa DLI alisema, “Hatimaye tumepata washindi wa shindano la Nne la DLI baada ya kupitia mchakato mrefu kutokana na kuwa tulikuwa na washiriki 41 waliotetea mapendekezo yao; miongoni mwao 9 wamechaguliwa washindi.” Aliongeza, “Tunashauku kubwa kuona mawazo yao yakibunifu yanakuwa tatuzi bora zitakazo saidia kutatua changamoto mbali mbali za kijamii na kuwa na matokeo ya moja kwa moja katika jamii zetu.”

Baada ya kuchaguliwa kama mmoja wa washindi, Bi. Linda Mlunde alisema, “Ninafuraha kubwa kwa DLI kunipa fursa hii.” Aliongeza, “Pia natarajia kulitekeleza wazo langu vizuri ili niweze kuleta matokeo chanya katika jamii yangu.”

Shindano la Ubunifu la DLI tayari limeshatoa ruzuku ya dola milioni 1.1 kwa washindi 37 kutoka madirisha matatu ya kwanza ya mashindano. Madirisha haya ya awali yalikuwa na lengo la kupunguza maambukizi ya VVU /UKIMWI na kuboresha huduma za afya kwa jamii ya Tanzania, pamoja na kuongeza ajira kwa vijana. Pata maelezo zaidi ya jinsi gani washindi hawa wanatumia takwimu/data katika kutatua changamoto za afya kupitia wasifu wa washindi kwa Shindano la Kwanza, Shindano la Pili, na Shindano la Tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.