22 watetea mapendekezo yao kwenye shindano la ubunifu la #ZeroHungerZeroAIDS

22 watetea mapendekezo yao kwenye shindano la ubunifu la #ZeroHungerZeroAIDS

Wabunifu wakitanzania watoa suluhisho la changamoto ya jinsi gani nchi inaweza kufikia lengo la kumaliza njaa na Ukimwi yaani #ZeroHungerZeroAIDS. Zaidi ya waombaji 180 walituma mawazo yao ya jinsi gani ya kutatua masuala yatokanayo na njaa na VVU/UKIMWI kupitia utumiaji wa data. Wiki hii, waliofikia hatua ya mwisho ambao ni 22 (taasisi 5 na watu binafsi 17) wametetea mapendekezo yao katika shindano la ubunifu lijulikanalo kama Zero Hunger Zero AIDS, ambao ni ushirikiano baina ya Data for Local Impact Innovation Challenge (DLIIC) na World Food Programme (WFP).

Shindano hilo la ubunifu la Zero Hunger Zero AIDS lilizinduliwa mnamo tarehe 20 mwezi wa Julai 2018 na kufungwa tarehe 7 mwezi Septemba 2018. Shindano hilo lililenga katika kuhakikisha kuwa kuna upatikanaji wa chakula cha kutosha chenye lishe bora na salama ili kupambana na changamoto za kiafya ikiwa ni pamoja na VVU/UKIMWI, na lilijikita katika maswali mawili maalum:

  1. Ni jinsi gani tunaweza fanya vyakula vyenye lishe kupatikana kwa urahisi zaidi, kwa bei nafuu na kuhitajika zaidi na watanzania, ikiwa ni pamoja na wanawake, watoto na wale walio katika hatari ya au wanaoishi na VVU/UKIMWI?
  2. Ni jinsi gani tunaweza wasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wao na kupigana na changamoto kama vile mabadiliko ya kimazingira na vihatarishi vya kiafya?

Akizungumza mara baada ya zoezi la uteteaji wa mapendekezo, Bw. Agapiti Manday, Meneja Mradi wa DLIIC, alisema kuwa dirisha la shindano la Zero Hunger Zero AIDS lilikuwa ni fursa kwa wabunifu wa kitanzania na wajasiriamali kutengeneza tatuzi katika maeneo ya uhifadhi wa chakula, lishe, kilimo bora na Vihatarishi vya kiafya – pamoja na VVU/IKIMWI.

“Tumepokea zaidi ya maombi 180 katika dirisha hili la shindano ambalo, baada ya hatua ya uchambuzi kufanyika, maombi 22 yalichaguliwa kuwa maombi ya mwisho kufikia hatua ya k utetea mapendekezo yao,” alisema Bw. Agapiti. Aliongeza, “Nje ya maombi 22, tunawanawake 7 na wanaume 15. Baada ya kusikiliza mawazo yao mazuri leo, tunaamini kuwa wabunifu hawa watakuja na ubunifu bora, utakaohakikisha kuwa kuna chakula cha kutosha, salama na chenye lishe bora na kuongeza uzalishaji katika kilimo, lakini pia kusaidia jamii ya watu yenye uhifadhi mdogo wa chakula kuzidi kujikinga dhidi ya vihatarishi vya kiafya, pamoja na VVU/UKIMWI.”

Bw. Agapiti pia alizungumzia juu ya ushirikiano wa DLIIC na WFP, shirika kubwa duniani linaloangazia katika utatuaji wa masuala ya njaa na kukuza uhifadhi wa chakula.  Alibainisha kuwa ushirikiano na WFP umeiwezesha DLIIC kuandaa mada za shindano zinazoangazia changamoto kubwa na za muda mrefu zilizopo katika jamii nchini Tanzania.

Akitoa maoni yake baada ya kupata nafasi ya kutetea pendekezo lake akiwa mmoja ya waliofikia hatua ya mwisho ya uteteaji wa mapendekezo, Bw. Paul Israel alisema, “Hii lilikuwa jukwaa zuri kwa vijana  wa kitanzania kuonyesha kuwa wana ujuzi lukuki na jinsi gani wao ni wabunifu, hususani katika eneo la maendeleo ya kilimo.” Aliongeza, “tatuzi nyingi zilizowasilishwa leo, zikiweza tekelezwa vizuri, zitakuwa na matokeo makubwa Tanzania, hasa katika maeneo ya vijijini.”

Shindano la Ubunifu la DLI limeshatoa ruzuku kwa washindi wapatao 37 kutoka katika madirisha matatu ya mwanzo, ambayo yalilenga katika kupunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI, uboreshaji wa huduma ya afya na uletaji wa uwezeshaji wa kiuchumi katika jamii za kitanzania. Soma zaidi jinsi gani washindi hawa wanatumia data katika kutatua changamoto hizo hapa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.