41 waitwa kutetea mapendekezo yao katika Shindano la Nne la DLI

41 waitwa kutetea mapendekezo yao katika Shindano la Nne la DLI

Kati ya maombi 344 yaliyopokelewa wakati wa dirisha la nne la mashindano, DLIIC ilichagua wahitimu 41 (wanawake 13 na wanaume 28) kufikia hatua ya juu. Wahitimu hawa 41 walitetea mawazo yao mbele ya jopo la majaji wataalam kutoka Wizara ya Afya na Ofisi ya Waziri Mkuu katika kitengo cha Uwezeshaji wa Vijana Kiuchumi. Tukio hili lilifanyika tarehe 11-13 Septemba katika ofisi za dLab Tanzania na liligubikwa na ubunifu wa hali ya juu.

Dirisha la nne la mashindano ya DLI lililenga matatizo katika ngazi ya jamii yaliyotambuliwa na wananchi wa kawaida kupitia mradi dada wa DLI, ujuliakanao kama Data Zetu, ambao unalenga kuchagiza matumizi ya takwimu/data katika ngazi ya chini ya jamii. Matatizo hayo yaliyotambuliwa yalizingatia maeneo makuu manne:

  1. Mimba za Utotoni
  2. Matumizi ya Madawa ya Kulevya
  3. Unyanyasaji wa kimwili/kijinsia
  4. Maendeleo ya Watoto

Matatizo haya ni matatizo yaliyopo katika jamii ya Tanzania, na yanaweza kushughulikiwa kwa kupitia ubunifu unaochagiza matumizi ya data, na kuambatana na vipaumbele vya PEPFAR katika kupunguza maambukizi ya VVU / UKIMWI.

Dirisha la nne la mashindano lilifunguliwa kwa ajili ya maombi tarehe 27 Aprili na lilifungwa Juni 27, 2018. Baada ya tathmini kufanyika katika miongoni mwa maombi 41 na matokeo ya uteteaji wa mapendekezo, washindi watapatiwa ruzuku na kwa upande wa watu binafsi/timu watapatiwa kuanzia Dola 10,000 – 25,000, wakati mashirika yatapokea ruzuku ya kuanzia Dola 75,000-100,000. Fedha hii ya ruzuku itatoleewa pamoja na msaada wa kiufundi kutoka timu ya mradi wa DLIIC.

“Tulipokea maombi zaidi ya 300 katika dirisha hili la shindano, lakini baada ya mchakato wa uchunguzi mapendekezo 41 yalikuwa kati ya mapendekezo bora na yenye vigezo vyote, alisema Bw. Agapiti Manday, Meneja wa Mradi wa DLIIC. Aliongeza, “Tuna matumaini kuwa kutoka kwa wahitimu 41 waliotetea mapeendekezo yao leo, tutaweza pata mapendekezo bora, sio tu kulingana na jinsi walitetea mapendekezo yao lakini kulingana na ubora wa wazo lililowakilishwa na uwezo wake wa kuleta matokeo chanya.

Akizungumza mara baada ya zoezi la uteteaji wa mapendekezo, Bw. Elias Mwinuka, mmoja kati ya washiriki waliofikia hatua uteteaji, alisema, “Ninafuraha sana kwamba nilipata fursa ya kuomba na pia kupata nafasi ya kuitwa kutetea pendekezo langu.” Aliongeza, “Ni vizuri kwamba tulianza na mafunzo kwanza ya jinsi ya kufanya uwasilishaji, ambayo yalitupa vidokezo vyema vya kile kilichohitajika kufanyika wakati wa uteteaji wa mapendekezo yetu.”

Kwa upande wake, Bi. Irene Swenya, ambaye pia ni miongoni mwa waliofikia hatua ya mwisho, alisema, “hii ndiyo mara yangu ya kwanza kuomba katika shindano hili la DLI na kuweza kupata nafasi ya kuja na kutetea….. kwa kweli hii kwangu ni nafasi ya kipekee. Aliongeza, “jambo jema ni kwamba, majaji walikuwa hawaulizi maswali tu, bali pia wanakusaidia kuliboresha wazo lako kuwa bora zaidi ili mwishoni mwa siku uweze kuunda suluhisho lililobora zaidi.”

Shindano la Ubunifu la DLI tayari limeshatoa ruzuku ya dola milioni 1.1 kwa washindi 37 kutoka madirisha matatu ya kwanza ya mashindano. Madirisha haya ya awali yalikuwa na lengo la kupunguza maambukizi ya VVU /UKIMWI na kuboresha huduma za afya kwa jamii ya Tanzania. Pata maelezo zaidi ya jinsi gani washindi hawa wanatumia takwimu/data katika kutatua changamoto za afya kupitia wasifu wa washindi kwa Shindano la Kwanza, Shindano la Pili, na Snindano la Tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.