Wabunifu wa DLI waonyesha matokeo ya miradi yao katika Wiki Ya Ubunifu Mwaka 2018

Wabunifu wa DLI waonyesha matokeo ya miradi yao katika Wiki Ya Ubunifu Mwaka 2018

Wiki ya Ubunifu kwa Mwaka huu wa 2018 (Ikifanyika kuanzia Mei 21-26) ilisisitiza “Ubunifu kwa Vitendo” na ilitoa jukwaa maalum lililowezesha ubunifu kuonekana ambao uleta matokeo chanya katika maendeleo ya binadamu. Tukio hilo la kipekee, liliandaliwa na taasisi ya Human Development Innovation Fund (HDIF) na lilifanyika katika ofisi za Tume ya Sayansi na Teknolojia ya Tanzania (COSTECH) jijini Dar es Salaam. Wiki hiyo ilipambwa na wabunifu wengi, ikiwa ni pamoja na washindi wa shindano la Ubunifu la Data for Local Impact Innovation Challenge (DLIIC), mradi unaofadhiliwa na MCC/PEPFAR.

Akizungumza juu ya tukio hilo, Meneja Muhamasishaji wa DLI Innovation Challenge, Bw. Collin Gumbu, alisema kuwa wiki hiyo ya ubunifu imefika kwa wakati muhafaka, wakati ambao DLI imefungua Dirisha la Nne la Shindano la Ubunifu, ambalo linalenga katika kutatua matatizo mbali mbali yaliyopo katika ngazi ya jamii kwa kutumia takwimu zilizopo katika jamii.

“Ilikuwa ni fursa ya kipekee kwetu kuweza kujenga uelewa juu ya dirisha la shindano letu la awamu ya nne, na ukizingatia mpaka sasa, dirisha bado liko wazi katika kupokea maombi. Tunategemea kutokana na uhamasishaji unaofanywa tutaweza kupokea maombi mengi kabla ya terehe ya mwisho, ambayo ni mwezi Juni tarehe 11, saa 4 alasiri, Saa za Afrika Mashariki,” alisema Bw. Collin.

Bw. Collin aliongeza: “Madirisha yetu mengi ya mashindano husisitiza upatikanaji wa tatuzi zakibunifu zitokanazo na takwimu kulingana na changamoto zilizopo katika jamii. Dirisha letu la sasa linalenga katika maeneo matano, yafuatayo: Mimba za utotoni, Matumizi ya madawa ya kulevya, Unyanyasaji wa kimwili na kijinsia, Maendeleo ya Watoto, na Vijana na Tatuzi zitokanazo na Takwimu, na naamini kwamba tutapata maombi mengi yatokanayo na kikao cha leo hapa katika Wiki ya Ubunifu kwa mwaka 2018. Kwa kweli ilikuwa ni fursa ya kipekee”.

Wakati wa kipindi cha DLI, washindi kutoka dirisha la kwanza na la pili la mashindano walipata fursa ya kuonyesha tatuzi zao za kibunifu.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuonyesha maendeleo ya mradi wake wa kibunifu, Bw. Mkata Nyoni, mmoja kati ya washindi wa dirisha la pili la DLI, alisema tatuzi yake katika eneo la  utoaji wa huduma za afya, iitwayo TANZMED, ipo katika hatua nzuri. Yeye na timu yake sasa wamejikita katika kujenga uelewa juu ya tatuzi yao, ambayo ipo katika mfumo wa App na Tovuti.

“Tuko katika hatua ambayo tunahitaji kuutangaza ubunifu wetu kwa kiasi kikubwa, kwa hiyo, wakati wowote tunapopata fursa ya kuonyesha maendeleo ya mradi wetu hatufikiri mara mbili katika kushiriki. Mimi na timu yangu, tunashukuru sana kualikwa na DLI katika Wiki ya Ubunifu kwa mwaka huu, na tunatarajia kupata fursa zaidi kama hii, ili tuutangaze ubunifu wetu ili watu wote nchi nzima waweze kufaidika, “alisema Nyoni.

Naye, Bw. Josephat Mandara, mmoja kati ya washindi wa dirisha la kwanza la  DLI, pia alipata fursa ya kuwasilisha maendeleo ta tatuzi yake ijulikanayo kama TausiJukwaa, ambayo imelenga kutatua changamoto za usafi wa hedhi kwa wasichana na wanawake vijana. Bofya hapa ili kufahamu zaidi juu ya TausiJukwaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.