Wabunifu 15 wajishindia ruzuku za Dirisha la Tatu la Shindano la DLIIC

Wabunifu 15 wajishindia ruzuku za Dirisha la Tatu la Shindano la DLIIC

Shindano la Ubunifu la Data for Local Impact Innovation Challenge (DLIIC) limetoa ruzuku kwa washindi 15 (Taasisi zikiwa 5 na Watu Binafsi 10) kupitia Dirisha la Tatu la Shindano la DLI, lililolenga kwenye eneo la Ajira kwa Vijana na Uwezeshaji wa Kiuchumi.

Wakati wa shindano, ambalo lilianza Desemba hadi Januari, maombi 365 yalipokelewa. Kutoka kwa waombaji hao, waliofikia hatua ya kuitwa ili kutetelea mapendekezo yao walikuwa 68. Shindano hilo lilijikita katika lengo namba 8 la Maendeleo la Maendeleo Endelevu, ambalo ukuza uchumi endelevu na jumuishi, ajira na kazi bora kwa wote. Kuhakikisha uwezeshaji wa kiuchumi na upatikanaji wa fursa, hasa kwa vijana, ni kipaumbele kikubwa kwa Tanzania. Uwezeshaji wa kiuchumi uchangia malengo mengine ya maendeleo, kama vile afya bora (ikiwa ni pamoja na kuondokana na tatizo la UKIMWI), usawa wa kijinsia, na kuondoa umasikini na njaa. Shindano lililenga maeneo yafuatayo:

  • Kuimarisha usawa kati ya mahitaji ya waajiri na ujuzi wa vijana; na kuandaa vijana kwa soko la ajira,
  • Kukuza uwezeshaji wa kiuchumi wa vijana, na
  • Kuendeleza na kuhamasisha muunganiko baina ya vijana na fursa za kiuchumi.

Dirisha la Tatu la shindano lilikuwa fursa kwa wajasiriamali wa ndani ili kuzalisha ubunifu mpya, teknolojia, na michakato mipya ya utumiaji wa data katika kushughulikia masuala ya kiuchumi na ajira yanayowakabili vijana wa Tanzania. Waombaji zaidi ya 365 waliwasilisha mawazo ya jinsi ya kuongeza uajiri wa vijana na uwezeshaji wa kiuchumi. Baada ya mapitio na tathmini ya kina, jopo letu la majaji ambao ni wataalam tofauti walichagua mapendekezo 68 ili kufikia hatua ya mwisho ya shindano – Waombaji Kutetea mapendekezo yao mbele ya majaji na hadhira.

Wakati wa tafrija hiyo, Bw. Makange Mramba, ambaye ni Mkuu wa Fedha wa taasisi ya Dar Teknohama Business Incubator (DTBi), aliwahimiza waliopkea ruzuku kuelekeza ruzuku hizo katika malengo yaliyokusudiwa, ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao.

“Ni heshima kubwa kwangu kuwa sehemu ya tukio hili la kipekee na kushuhudia DLI ikijenga historia tena kwa kufikia hatua hii muhimu kwa kuwajengea  mazingira mazuri vijana ya upatikanaji wa ajira na uwezeshaji wa kiuchumi kupitia matumizi ya data/takwimu na ubunifu,” alisema Bw Mramba.

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa DLIIC, Bw. Agapiti Manday, alisema anasubiri kwa hamu kubwa kuona nini kitatokana na mawazo mazuri ya kibunifu toka kwa washindi wa Dirisha la Tatu la DLI.

“Wamekuja na mawazo yakipekee kabisa, ya kibubunifu katika kutatua masuala ya ajira kwa vijana na changamoto za uwezeshaji wa kiuchumi, na tunatarajia kuona mawazo haya ya kibubunifu kuwa tatuzi zitakazosaidia kuleta matokeo chanya katika jamii yetu kwa ujumla,” alisema Bw. Agapiti.

DLIIC mpaka sasa imeshatoa ruzuku kwa washindi 22 kutoka katika Shindano la Kwanza na la Pili. Madirisha haya mawili ya mashindano yalilenga katika kupunguza hatari za VVU / UKIMWI na kuboresha huduma za Afya kwa Jamii za Tanzania. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi gani washindi wa DLIIC wanavyotumia data/takwimu katika changamoto za Afya kwa kutembelea Wasifu wa Mshindi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.