Wafadhili katika Sekta ya Ubunifu waaswa kujitokeza kuwekeza katika miradi endelevu itokanayo na takwimu/data

Wafadhili katika Sekta ya Ubunifu waaswa kujitokeza kuwekeza katika miradi endelevu itokanayo na takwimu/data

DLIIC inazindua shindano jipya la ubunifu kwa miradi endelevu ikiwa ni jitihada madhubuti za kuendelea kuwaunga mkono wale waliopokea ruzuku  na waliofanikiwa kukamilisha hatua muhimu katika mradi yao, kutengeneza tatuzi zao zilizoanza kufanyakazi, na kupata msaada wakifedha kutoka kwa mshirika wa nje. Tunatafuta washirika wan je na wafadhili ikiwa ni pamoja ma Serikali, wafadhili, sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, au watu binafsi, ambao wataweza kutoa asilimia 25 mpaka 50 ya fedha na DLIIC watatoa fedha zilizobaki. Hii ni fursa yakipekee ili kusaidia kukuza matokeo chanya ya tatuzi ambazo tayari zimeanza kufanya kazi.

Ruzuku karibia zote 22 zilizotolewa na DLIIC hadi sasa zimetolewa kwa watu binafsi au timu zilizo na mawazo mapya, badala ya utoaji wa ruzuku ili kuendeleza miradi ya kibunifu iliyopo. Wengi kati ya wale waliopokea ruzuku wamefanikiwa kutengeneza miradi yao na kufikia katika hatua nzuri na kuweza kuaminiwa na watu kutoka serikali za mitaa na NGO’s. Kutokana na hamasa itokanayo na miradi hii, DLIIC inataka kupanua kasi ya huo ubunifu ili kuwasaidia  washindi ambao wamefanya vizuri katika utekelezaji wa hatua za awali za miradi yao yakibunifu, kwa kuwaleta wafadhili na wawekezaji wengine washirika ndani ya mradi.

Vigezo vinavyohitajika kwa ajili ya uombaji wa fedha katika miradi endelevu ya DLIIC yaani Scale – Up Funds:

  • Mfano wa kazi na kupima mafanikio na ushahidi wa dhana
  • Uwezekano wa kuwa endelevu / uendelezaji
  • Umeonyesha usimamizi nzuri wa kifedha
  • Uendane na hitaji la Kijiografia – Yaani miradi ilenge wilaya zilizopewa kipaumbele na PEPFAR na Global Fund
  • Upatikanaji wa washirika wenye nia na ufadhili wa ushirikiano

Ikiwa wewe ni mfadhili, mwekezaji, serikali au shirika la watu binafsi, lenye nia ya kuingia kwenye sekta ya ubunifu, hii ni fursa ya kipekee ya kuwekeza kwenye ubunifu wa kijamii uwezao kuleta mabadiliko chanya ya muda mrefu yanayochangia katika ukuaji wa kiuchumi, uboreshaji wa afya na ukuzaji wa masuala ya usawa wa kijinsia.

DLIIC inaweza kufanya nini kwa wabunifu? Fursa zaidi za kifedha zinakuja tukiwa tunajiandaa na madirisha mawili yaani la Nne na la Tano. Jisajili ili upate jarida letu, pia ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii, na tembelea kurasa yetu ya maombi ili uendelee kupata taarifa au matangazo muhimu juu ya mashindano yetu ya kibunifu.

  

Kuhusu DLIIC

Shindano la Ubunifu la Data for Local Impact Innovation Challenge (DLIIC) linatambua, watu wa kushirikiana nao, na kuwasaidia vijana na wajasiriamali kutengeneza tatuzi zitokanazo na takwimu/data kwa ajili ya matatizo yaliyopo katika jamii. Kama sehemu ya kazi hii, DLIIC inaandaa madirisha ya mashindano ya kibunifu yanayokuza matumizi ya takwimu katika uboreshaji wa afya, kuwalinda wasichana na kuwawezesha vijana. Katika 2017, DLIIC ili watambua na kutoa ruzuku zipatazo 22 katika madirisha mawili. Kundi la kwanza la wapokea ruzuku lilimaliza miradi yao mnamo Novemba 2017, na la pili likitegemea kumaliza hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published.