Mbali na fedha na msaada wa kiufundi, DLIIC humpatia mpokea ruzuku wake mshauri au huduma ya huduma ya ushauri. Wanaume na wanawake ambao hutumiwa kama washauri wa DLIIC wana uzoefu mkubwa katika nyanja mbalimbali, kutoka uhandisi wa umeme mpaka kwenye afya ya uzazi hadi mawasiliano na sayansi ya kompyuta. Kila mshauri huleta mtazamo wa pekee na ujuzi wa kushauriana. Jifunze zaidi kuhusu wanaume na wanawake ambao wanatoa msaada kwa kizazi kipya cha wavumbuzi kwenye ukurasa wetu wa Washauri.
Katika maneno ya uchambuzi, DLIIC ina aina tatu za washauri: Mshauri kwa mtu mmoja mmoja, washauri wataalamu na washauri waandamizi. Kila mmoja utumikia kwa kusudio tofauti katika mzunguko wa ubunifu na uvumbuzi.
Mshauri kwa mtu mmoja mmoja
Hawa ni washauri ambao ukutana mara kwa mara na kushawishi wabunifu moja kwa moja wakati wa kipindi cha ruzuku cha DLIIC. Mshauri mmoja kwa wakati mwingine anaelezewa kuwa ‘rafiki muhimu’ kwa sababu anaelezea kazi ya mbunifu na wakati mwingine uwahimiza kufanya kazi kwa bidii. Washauri hawa wanaweza kuitwa kufanya kazi mbalimbali, kulingana na mahitaji ya wabunifu.
Majukumu haya ni pamoja na:
- Kuwafanya wavumbuzi kufahamu matatizo ama mambo ambayo awali walikuwa hawayafahamu.
- Kuwa mvumilivu
- Kuwa na uwezo mkubwa
- Kutoa ushawishi yakinifu
- kutoa ushauri wa tahadhari wakati unapohitajika
- Kutoa uunganisho na mawasiliano muhimu
Watu wanaofanya jukumu hili upatiwa mafunzo na kusimamiwa na Mshauri Mkuu wa DLIIC na Afisa wa Ushauri wa DLIIC. Wana ufahamu mzuri wa eneo litomikalo katika ubunifu, ujuzi wa mchakato wa ubunifu au utaalamu katika usimamizi wa mradi ama yote matatu.
Mshauri Mtaalam
Inaweza kusaidia kuwajumuisha mshauri mmoja mmoja na mshauri mtaalamu. Washauri hawa wamefundishwa katika mbinu sawa ya ushauri kama mshauri mmoja mmoja, isipokuwa kwamba lengo ni juu ya eneo maalum kama VVU / UKIMWI, elimu, afya, ujana, au maendeleo ya programu. Usimamizi wa DLIIC uhamua wakati mshauri wa kitaalamu anahitajika kusaidia kwa kutatua changamoto zinazomkabili mpokea ruzuku. Mshauri Mtaalamu ujenga kujitegemea kwa wabunifu kwa mtindo wa kutokuwaonyesha mojakwamoja chakufanya bali (kuwaongoza badala ya kuwaambia nini cha kufanya).
Mshauri Mwandamizi
Watu hawa wana uzoefu wa kutosha wa ushauri wa kufanya kazi kama washauri kwa washauri wapya ambao hawana ujuzi. Wakati washauri wapya wana nafasi ya kufanya kazi na mshauri mwandamizi, pia wanapata ujuzi na utaalamu.
Ushauri wa Pamoja
Mbali na kuwapa wapokea ruzuku mshauri mmoja kwa moja, DLIIC imeunda utaratibu ambao unaweza kutajwa kuwa “vikao vya kushauriana pamoja”. Vikao hivi vinahusisha washauri wengi na kuwakilisha fursa kwa wapokea ruzuku kutoa maoni juu ya maendeleo ya miradi yao ya uvumbuzi na kupata maoni kutoka kwa timu ya wataalamu na washauri waliochaguliwa kwa makini. Utaratibu huu umethibitishwa sana kwa wabunifu ambao wanafaidika na utofauti wa mawazo na uzoefu ambao vikao hivi vinautoa.
Je, una ujuzi na utaalamu gani unaotaka kuutoa kwa kizazi kijacho cha wavumbuzi na wajasiriamali? Ikiwa uko tayari kuwa mshauri, tunataka kusikia kutoka kwako! Wasiliana na Mwasiti Mkembe kupitia barua pepe: info@dli.teknohama.or.tz
Leave a Reply