MRADI wa Data for Local Impact Innovation Challenge (DLIIC) ni wa kitaifa ambao unaungwa mkono na washirika kadhaa ili kuwasaidia vijana kujifunza jinsi ya kuwa wabunifu. DLIIC hutoa msaada kwa wabunifu ambao hutumia takwimu kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa athari za kimaisha ambazo mara nyingi huwa zinawakabili wasichana na wanawake wenye umri mdogo. Hata hivyo kama ilivyo katika shughuli za biashara, miradi mingi ya wabunifu inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kudumu na kuwa endelevu. Ili kuongeza nafasi za mafanikio na kuwa njia za mfano, DLIIC hutoa ushauri kwa wabunifu kutumia mbinu mbadala za nadharia na vitendo. Na matokeo yake miradi 10 kati ya 12 imefanikiwa kukamilika na baadhi yake tayari ina mafanikio makubwa.
Mshauri maana yake ni nini?
Maana ya neno mshauri linatokana na maudhui ya lugha ya Kigiriki ‘.Neno hili lipo katika moja ya tenzi za ushahiri ambalo aliutunga Odysseus kabla ya safari yake ya Epic, ambapo alimfanya mwanawe kuwa chini ya uangalizi wa rafiki yake mshauri wa zamani ambaye alikuwa akimwamini. (Alikuwa ni mwanamke aitwaye Goddess Athena).
Hata hivyo ushauri wa kisasa unategemea dhana ya kujifunza, ambapo mtu mwenye ujuzi zaidi uushusha chini kwa wenzake ili kuwafundisha jinsi ya kufanya kazi katika ulimwengu wa kibiashara.
Ufuatilia ndicho kiini cha msingi wa maendeleo ya binadamu ambacho uwaongezea tamaa ya kujifunza na kuwasaidia wengine kuimarika na kutimiza ndoto zao. Mifano mingi ya uhusiano wa kimafunzo upo katika tamaduni tofauti kama vile Guru nchini India, Mwalimu nchini China, na Mzee wa Kijiji nchini Afrika.
Ushauri mara nyingi unalinganishwa sawa na huduma za usaidizi kama vile kufundisha. Wakati mwingine maneno haya mawili hutumiwa kwa pamoja. Ijapokuwa ufafanuzi wa “kufundisha” na “ushauri” hutofautiana katika mazingira tofauti na tofauti yake tunaiweka kama ifuatavyo: Ushauri una lengo la muda mrefu ambalo ni la kupanua mtazamo wa mtu na msimamo wake. Maana hii inasisitiza mtu kujitegemea na kujiamini katika malengo yake . Kwa upande wa kufundisha maana yake ni lengo la muda mfupi na linalenga kuboresha ujuzi maalum, ujuzi au tabia zinazohusiana na biashara ya kila siku ya mwanadamu.
Katika DLIIC, ushauri unaweza kuelezewa kama ushirikiano kati ya watu wawili ambao wana ngazi tofauti za uzoefu. Mshauri hutoa msaada na fursa za maendeleo na jinsi ya kukabliana na masuala ya changamoto (kutambuliwa na mshauri au mshauriwa). Ushauri ni shughuli nzuri katika maendeleo na sio msaada wa kielimu. Ushauri wa DLIIC umeundwa kama washauri waajiriwa na wanafundishwa kulingana na malengo ya mradi na mfumo wake. Wakati huo huo, wapokea ruzuku wa DLIIC katika programu hii wamefundishwa juu ya maana na malengo ya ushauri na juu ya majukumu yao katika uhusiano huo.
Awamu tatu muhimu za Ushauri wa DLIIC
Wapokea ruzuku wa DLIIC wanapaswa kukamilisha awamu tatu katika mradi wao wa ubunifu. Uhusiano wa DLIIC wa mshauriwa na mshauri unafanyika kufuatilia hatua hizi tatu muhimu, ambazo wapokea ruzuku uendanazo na kuzipitia katika kila awamu.
Awamu ya Kwanza : Wapokea ruzuku ukusanya taarifa kutoka kwa wadau mbalimbali ambao wanaweza kufaidika na ubunifu wao. Taarifa hii hutoa msingi kwa wapokea ruzuku ambao unaweza kusaidia kuchunguza masuala mapana ambayo mvumbuzi anapaswa kuzingatia wakati wa kuendesha mchakato wa kutafuta suluhisho ambalo litashughulikia changamoto za jamii kwa kutumia takwimu . Hatua hii inaisha wakati mpokea ruzuku akijiandaa kutengeneza mchoro wa pendekezo lilitolewa na mbunifu katika kutafuta ufumbuzi wa ili kuendelezwa. Katika hatua hii, washauri husaidia wapokea ruzuku kukusanya na kuchambua taarifa za kutosha na zinazofaa.
Awamu ya Pili: Katika awamu hii wapokea ruzuku hutoa suluhisho la ubunifu ambalo walilitengeneza kwa kutumia ruzuku za DLIIC. Wakati huu, wapokea ruzuku huwa wanakabiliwa na changamoto ya kuendana na muda ambao umewekwa ili kukamilisha mfano wa suluhisho.
Wakati huo wapokea ruzuku wanakuwa makini na mradi wao na kutatua changamoto zitakazoweza jitokeza wakati wa ubunifu na utekelezaji wa mradi, ambapo vyote ni vitu vipya kwa washauriwa. Kama wapokea ruzuku inapokaribia mwishoni mwa hatua hii ni muhimu kwa mshauri kuanza kufikiri juu ya kuumaliza uhusiano.
Awamu ya Tatu: Katika awamu hii ubunifu wa mpokea ruzuku… unadhaniwa kumalizika ambapo unatoa majibu ya changamoto zilizopo katika jamii na kumridhisha mbunifu. Katika hatua hii, wapokea ruzuku uleta ubunifu wao (tatuzi zao) kwa watumiaji waliokusudiwa ili kupata maoni yao. Ushauri katika hatua hii, unajumuisha, kati ya mambo mengine, majadiliano ya makusudi ya kukuza kujitegemea kwa mshauriwa na kumtayarisha kijitegemea. Mazungumzo haya ni muhimu ili kuhakikisha kuwa mbunifu amejiandaa kikamilifu kwenda ‘kujitegemea’ na kuzuia mtu kumtegemea mwenzake baada ya kipindi cha ushauri kuisha.
Ushauri ni sehemu muhimu ya jitihada za DLIIC kusaidia vijana na wajasiriamali kuunda tatuzi-zitokanazo na takwimu zinazoendena na matatizo halisi ya watu. Washauri wetu tayari wameshawasaidia washindi 12 waliokuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili katika kukamilisha miradi yao, na sasa wanawasaidia washindi 10 kupitia Dirisha la 2 la shindano.
Leave a Reply