Je unafahamu jinsi ya kufanya uwasilishaji?

Je unafahamu jinsi ya kufanya uwasilishaji?

Je unafahamu jinsi ya kufanya uwasilishaji?

Je una wazo la ubunifu, ambalo litabadilisha sekta na kusaidia watu wengi. Vizuri! Sasa unawezaje kumshawishi mtu ili aweze kuwekeza katika wazo lako?
Inawezekana kwamba wakati fulani, utahitaji “kuwasilisha wazo lako” kwa wawekezaji. Unapowasilisha wazo lako kwa wawekezaji, utawatupia wazo lako kwao na unatarajia watalipokea, watalipenda na kuwekeza. Sehemu ya shindano la ubunifu la DLI ni tukio la uwasilishaji wa pendekezo lako, ambapo jopo la majaji watanzania waliobobea litathmini na kutoa maksi kwenye mawazo ya washiriki wetu. Washiriki wetu wanapewa dakika 5-7 kufupisha mawazo yao na kuwashawishi majaji kutoakana na mawazo yao. Huu sio muda wa kutosha, kwa hiyo wanapaswa kuhakikisha uwasilishaji wao unalenga maeneo muhimu na nirahisi kuwavutia hadhira. Tuna vidokezo vitakavyo wasaidia washiriki kuandaa uwasilishaji wao, na tunapenda kuwajuza.
Ni nini maana ya “Pitch Deck”, ni maelezo mafupi yaliopo katika uwasilishaji, yanayotoa muhtasari wa wazo lako na mpango wako wa kibiashara kwa hadhira. Unaweza tumia Pitch Deck wakati wa mikutano ya uso kwa uso au mtandaoni na wawekezaji, wateja, au washirika. Washiriki wetu walio wengi utumia Slide Deck ili kusaidia uwasilishaji wa mapendekezo yao. Hapa, tunakupatia vidokezo kadhaa vya jinsi gani ya kutengeneza Slide Deck nzuri na yenye kushawishi!

DLIIC Pitch Presentation Tips

 

Watu wengi wanaogopa kuongea mbele ya hadhira, lakini kama uwezi kuwasilisha mawazo yako kwa kujiamini, utakuwa na wakati mgumu wa kumshawishi mtu kuwekeza juu yako. Hapa, tunakupatia vidokezo vichache kukusaidia ujisikie na ufanye kwa kujiamini wakati unawasilisha mawazo yako:

 

DLIIC Public Speaking Tips

Leave a Reply

Your email address will not be published.