DLIIC katika mchakato wa kutafuta wabunifu ili kupambana na changamoto za afya nchini Tanzania
Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, Serikali ya Tanzania imekuwa na maendeleo mazuri katika kufungua vituo vya takwimu ili kuweza kuweka uwazi mkubwa na kuongeza ufanisi kiutendaji. Hata hivyo pamoja na jitihada hizo za serikali kuna fursa nyingine ya kuhusisha zaidi jamii na kuijengea uwezo kiufundi kwa kutumia habari ili iweze kushughulikia kikamilifu vipaumbele vya taifa.
Hadi sasa wabunifu 12 wameweza kupewa ruzuku kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi katika masuala ya afya nchini Tanzania kupitia mpango wa maalumu unaoitwa Local Impact Innovation Challenge (DLIIC) unaofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia mpango wa dharura wa Rais kwa ajili ya kushughulikia masuala ya UKIMWI (PEPFAR).
Kupitia mpango huo, Wajasiriamali hawa watapata fedha kuanzia dola za Marekani 7,000 hadi dola 25,000, na msaada wa kiufundi pamoja na ushauri ili waweze kutekeleza fumbuzi wa aina mbalimbali katika masuala ya kijamii.
Mapendekezo ya kushindanisha yanajumuisha ufumbuzi unaofaa kusaidia wananchi kupata habari za huduma za afya, kupunguza upungufu wanawake na wasichana wadogo mashuleni ambao unaosababishwa na changamoto za afya, kuwezesha kugawana taarifa juu ya ubora wa huduma za afya, na kuongeza matumizi ya wananchi ya kumbukumbu za Serikali ya Tanzania (Daftari la Usajili wa Afya au HFR).
Mapendekezo ya kushindanisha yakiwa yameambatanishwa na jina la kiongozi wa timu kulingana na mada yao kuu ni kama ifuatavyo:
*Upatikanaji wa Huduma za Afya Bora na Taarifa
Jackson Machael Ilangali
Musa Sendama Kamata
Bukhary Haruna Kibonajoro
Rahim Abas Kiobya
George Elly Matto
Mohammad Abdulghany Himidi Msoma
*Maoni kutoka kwa jamii
Steven Edward Mangowi
Rachel Samuel Nungu
*Uwezeshaji kwa wananchi
Lulu Said Ameir
Rose Peter Funja
Jonathan Manyama Kifunda
Josephat Geofrey Mandara
Mapendekezo 12 yalichaguliwa kutoka katika maombi 129 baada ya kupitiwa na jopo huru la wajasiriamali wa Tanzania, wavumbuzi na wataalamu wa afya kulingana na uwezo wao wa kuboresha aidha au mahitaji ya takwimu.
Mapendekezo yalitakiwa kuzalisha au kutumia taarifa au takwimu zilizowazi ambazo zimefanya kazi ndani ya miezi mitatu, na kuzingatia masuala yanayowakabili vijana, wanawake wadogo na jamii kwa ujumla.
Ufumbuzi wake pia ulitakiwa kulenga angalau moja ya wilaya 84 ambazo zinazingatia vipaumbele chini ya PEPFAR 2017 Mpango wa Uendeshaji wa Nchi Tanzania (COP), ulioandaliwa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
“Mpango huu wa (DLIIC) una lengo la kushiriki, kusaidia, na kuunganisha wabunifu wa Watanzania, watengenezaji na watoa ufumbzi kwa kila mmoja na pia kutoa fursa ya kuondoa tofauti katika jamii,” anasema Agapiti Manday ambaye ni Meneja wa Programu ya DLIIC.
DLIIC inakusudia kuwajenga vijana kikamilifu, ili kuimarisha matumizi yao ya takwimu na uwezo wa sayansi ya takwimu na kuchangia lengo la PEPFAR la kuleta ushiriki mkubwa wa wananchi katika kudhibiti, na hatimaye kulimaliza janga la UKIMWI.
Washindi wataanza mafunzo yao wiki ya kwanza ya Machi 2017, na watafanya kazi katika kutekeleza miradi yao zaidi ya miezi 3-6.
Watakuwa sehemu ya mpango wa ujasiriamali ambao utaimarisha ujuzi wao wa usimamizi wa miradi, biashara binafsi na uwezo wa kutumia sayansi ya kumbukumbu. Jambo muhimu zaidi kwa wabunifu hawa watakaoshinda wataweza kusambaza maana ya ubunifu katiika jamii zao ili kuondoa mambo ambayo yanaathiri maisha ya Watanzania.
Leave a Reply