Baada ya mashindano mawili yaliyofanikiwa, Data for Local Impact (DLI) Innovation Challenge ipo katika mkakati wa kuandaa Shindano la Dirisha la Tatu. DLI ilifanya shindano lake la dirisha la pili mnamo mwezi Mei 2017 baada ya shindano la kwanza mwezi Oktoba 2016. Wakati shindano la likiangazia masuala ya uboreshaji afya na dirisha la pili likilenga jinsi gani ya kuwalinda wasichana na wanawake vijana dhidi ya UKIMWI, Dirisha la tatu la litaangazia katika masuala ya Uwezeshaji wa Kiuchumi, Ajira ya Vijana na Lengo namba 8 la Maendeleo Endelevu. SDG8 linalenga zaidi ukuzaji wa uchumi endelevu, na jumuishi, ajira kamili na zalishaji pamoja na kazi bora kwa wote.
Shindano la Ubunifu la DLI linaunga mkono Malengo ya Maendeleo Endelevu na linalenga kuchangia maendeleo katika maeneo ya Afya na Ustawi (SDG3), Usawa wa Jinsia (SDG 5) na Kazi Bora na Ukuaji wa Uchumi (SDG8).
Shindano hilo jipya linaendana na lengo la DLI ambalo dhumuni lake ni kushirikisha, kusaidia, na kuunganisha wabunifu, waandaaji, na watoa ufumbuzi wa Tanzania ili kuleta utofauti katika maisha ya watu kwa kuongeza matumizi au upatikanaji wa takwimu/data. Kwa maana hiyo, timu ya DLI inahimiza wabunifu wote wa Tanzania kuzungumzia juu ya mada hiyo na kuleta mawazo yao thabiti dhidi ya changamoto katika masuala ya Uwezeshaji Kiuchumi, Ajira kwa Vijana na Lengo namba 8 la Maendeleo Endelevu.
Washindi katika shindano la Ubunifu la DLI wanapokea ruzuku ili kuwawezesha kuendeleza mapendekezo yao ya ufumbuzi kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sita. DLI inatoa ruzuku kwa watu binafsi au timu kuanzia Dola za Kimarekani 10,000 hadi 25,000 (Kama Shilingi za kitanzania milioni 25 hadi 50) pamoja na ruzuku kwa taasisi kuanzia Dola za Kimarekani 75,000 hadi 100,000 (Kama Shilingi za Kitanzania milioni 150 hadi 215). Washindi pia uunganishwa na washauri wao, ambao uwasaidia kuendeleza mawazo yao ya kibunifu kuwa moja kwa moja bidhaa ya mwisho. Pia wanapatiwa mafunzo na msaada wa jinsi gani ya kutumia ruzuku zao kutoka katika timu ya DLI.
Hivyo, DLI inafungua mlango kwa watanzania wote wenye kuthubutu na wanaotaka kuleta mabadiliko katika maisha ya watanzania wenzao kupitia ubunifu wao wa jinsi gani ya kutumia au kuunganisha takwimu/data, ikiwa ni pamoja na data zilizowazi. Kwa wale wenye nia, tafadhali watembelee tovuti ya DLI kwa ajili ya kupata taarifa juu ya tarehe za uanzaji wa shindano na vidokezo zaidi juu ya shindano hilo.
Je ungependa kushiriki? Ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii ujifunze kuhusu data, shindano la tatu na fursa nyingine za ufadhili wa fedha katika masuala ya data na ubunifu. @DLIInnovation, @dLabTZ, @datazetu, #InnovationTZ, #DataRevolutionTZ #LocalDataUse and #OpenData.
Leave a Reply