Katika Dunia nzima, wafadhili na wawekezaji wanatambua umuhimu mkubwa wa “Mifuko ya Ubunifu” na “Mashindano ya Kibunifu” ili kuwatambua wajasiriamali walio wabunifu, mawazo yenye mchango mkubwa katika kutatua matatizo yaliyokithiri katika jamii, ikiwa ni pamoja na afya, maji na usafi wa mazingira, elimu, haki za kijamii, na usawa wa kijinsia.
Miongoni mwa mifuko hiyo, DLI Innovation Challenge haiku peke yake katika jitihada zetu za kutumia data yaani takwimu katika uwekezaji wetu. Global Partnership for Sustainable Development Data na Benki ya Dunia yaani World Bank hivi karibuni walizindua mfuko wa kibunifu ujulikanao kama ‘Leave No One Behind’ wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 2.5. Mpango huo mpya umelenga katika kuboresha upatikanaji na utumiaji wa data/takwimu, na kuhitaji mapendekezo yanayolenga kuboresha takwimu katika nchi maskini dhidi ya watu wenye ulemavu na waliotengwa kama vile watu wasiokuwa na makazi, wakimbizi na katika changamoto zinazohusiaka na mabadiliko ya hali ya hewa na uhamaji katika maeneo ya miji.
“Tunatafuta ushirikiano unaoangazia mwanga kwenye vikundi ambavyo vilikuwa vimeachwa kihistoria na uchunguzi wa jadi na mifumo mingine ya ukusanyaji takwimu, alisema Claire Melamed, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Partnership for Sustainable Development Data. “Utengwaji upo wa namna nyingi, na ili usimuache yoyote nyuma ‘Leave No One Behind’ ni lazima tuwekeze katika takwimu/data bora ili kufanya maamuzi mazuri yatakayopelekea kuwa na maisha mazuri.”
Mfuko huu wa ubunifu umelenga katika mapendekezo yanayolenga katika kuboresha uzalishaji wa data/takwimu, utoaji wake, na matumizi yake katika nchi zenye kipato cha kati na chini, na katika miradi ambayo inawaleta pamoja wadau mbali mbali kuzungumzia matatizo makubwa. Timu zitakazofanikiwa zitapatiwa ruzuku ambazo ni kati ya Dola za Kimarekani 25,000 mpaka 250,000. Mapendekezo katika mzunguko wa kwanza yatakiwa kutumwa kabla ifikapo Tarehe 1 Septemba 2017 na kutumwa kupitia mfumo uombaji wa kimtandao.
Kwa Taarifa zaidi juu ya fursa hii ya ufadhili, tafadhali tembelea: https://wb-gpsdd-datainnovation.forms.fm/call-for-proposals-collaborative-data-innovations-for-sustainable-development
Mobile for Development (M4D) Utilities Innovation Fund ni mpango unaolenga kusukuma teknolojia ya simu za mkononi na takwimu katika kuunga mkono Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa kuboresha au kukuza upatikanaji wa nishati, maji na huduma za usafi wa mazingira. Awamu ya pili ya M4D sasa imefunguliwa ikiwalenga wajasiriamali, watoa huduma mbali mbali na MNOs ambao wanatumia teknolojia ya simu za mkononi kusaidia kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) namba sita na saba. Dirisha la shindano litafungwa ifikapo tarehe 3 Septemba 2017. Kwa taarifa zaidi tembelea: https://www.gsma.com/mobilefordevelopment/programmes/m4dutilities/innovation-fund-2
Leave a Reply