Dk. Afua Mohamed

Dk. Afua Mohamed

Dk. Afua Mohamed ana shahada ya uzamifu ya teknolojia katika uhandisi wa umeme kutoka Chuo Kikuu cha Cape Peninsula huko Cape Town, Afrika ya Kusini. Alikamilisha na shahada ya uzamili katika uhandisi wa umeme na ufundi, akijikita zaidi katika eneo la mashine za umeme na udhibiti.

Dk. Mohamed kwa sasa anafanya kazi katika Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kama afisa mwandamizi utafiti katika kurugenzi ya ubunifu, ujasiriamali na ushindani. Pia ni mratibu wa ofisi za COSTECH Zanzibar. Akiwa kama afisa mwandamizi utafiti, anaratibu utafiti, teknolojia na ubunifu nchini na Zanzibar.

Kabla ya kujiunga na COSTECH alifanya kazi kama mhadhiri katika taasisi ya teknolojia Dar es salaam na ana uzoefu wa miaka kumi na sita ya kufundisha  masomo tofauti katika umeme, mawasiliano ya simu na idara ya uhandisi kompyuta.

Amekua akisimamia, akiratibu, akielekeza na kushauri wanafunzi wa uhandisi katika miradi na tasnifu zao. Pia alihusishwa katika kupitia makaratasi yao ya kisayansi na hoja katika umeme na maeneo yanayoendana. Alijihusisha na masomo tofauti ya utafiti na miradi na kufanya kazi katika kamati mbalimbali kama katika Tume ya teknolojia ya habari na ofisi za mkuu wa takwimu (OCGS).

Maslahi yake ya utafiti ni katika usimamizi wa nishati ya umeme hasa katika sekta ya viwanda katika eneo la marekebisho ya nguvu na vifaa vya ufanisi wa nishati kama mitambo ya ufanisi nishati na mita erevu.

Profile details

Leave a Reply

Your email address will not be published.