Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

DLIIC imepokea zaidi ya maombi 340 katika dirisha la nne la shindano. Majaji wamekuwa wakiendelea kupitia mapendekezo hayo na kuchagua yale yenye mawazo bora kwa ajili ya tukio muhimu la mwisho la kutetea maombi yao. Tunategemea kutangaza washindi mwezi Oktoba 2018.

DLIIC imepokea zaidi ya mapendekezo 180 katika dirisha la tano la shindano. Majaji wamekuwa bize wakipitia mapendekezo hayo na kuchagua mawazo bora kwa ajili ya hatua ya kuyatetea katika tukio lijulikanalo kama Sahara Sparks. Tunategemea kutangaza washindi Mwezi Novemba 2018.

Baada ya kupitia maombi yote yaliyo na vigezo, DLIIC itawasiliana na waombaji kwa kupitia barua pepe na kuwataarifu juu ya maombi yao. Waombaji wasiofanikiwa watataarifiwa kuwa wameshindwa kuendelea kwenye hatua inayofuata. Tunawashawishi waombaji wote wasiofanikiwa kuendelea kuwasiliana nasi kupitia mitandao yetu ya kijamii ili kujifunza juu ya fursa nyingine za ruzuku. Waliofikia hatua ya mwisho wanaalikwa kufika DLI na kutetea mapendekezo yao mbele ya jopo la majaji wazalendo. Baada ya tukio la kutetea mapendekezo yao, washindi pia watataarifiwa kupitia barua pepe.

DLIIC haina mkakati wa kutangaza dirisha lingine la shindano. Mradi wa DLIIC utarajia kuisha ifikapo mwezi Desemba 2018. Hata hivyo, kazi za DLIIC zitaendelea kufanyika kupitia Tanzania dLab NGO. Hii itakuwa ni pamoja na mashindano yajayo ya kibunifu! Tembelea www.dlab.or.tz kujua zaidi juu ya dirisha lijalo la shindano. Mpaka hapo, endelea kuifuatilia DLIIC kwenye mitandao ya kijamii ili kupata fursa mbalimbali za misaada ya kifedha kutoka dunia nzima.

DLI Innovation Challenge hufadhiliwa na PEPFAR kupitia mpango wa MCC-PEPFAR DCLI na unalenga katika jitihada zinazohusiana na Afya na Ustawi (SDG 3), Usawa wa Jinsia (SDG 5), na Kazi Bora na Ukuaji wa Uchumi (SDG 8). Kabla ya kila dirisha la shindano, DTBi inatumia mchakato shirikishi na ushirikiano na wadau wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya serikali husika na taasisi nyingine zinazohusiana na eneo husika la shindano. Orodha ndefu ya mada kuu hupitiwa, kurekebishwa, kuendelezwa na kupimwa wataalam husika kabla ya kuchagua mada kuu za mwisho za shindano.

Baada ya kutuma maombi yako, utapokea barua pepe ya uthibitisho wa utumaji wa maombi yako na kukupa fomu ya maombi yako katika mfumo wa PDF. Endapo haujapokea uthibitisho huu kwa barua pepe, wasiliana nasi kupitia info@dli.teknohama.or.tz kwa msaada zaidi.

DLIIC inafuata mfumo uliokwisha wekwa, wa kupitia maombi na kuchagua washindi. Kwanza, DLIIC inafanyia tathmini na kupitia maombi yote kulingana na vigezo vilivyowekwa. Maombi yote yenye vigezo baada ya hapo yanapitiwa na timu ya mradi ya DLIIC kwa kutumia vigezo vilivyowekwa. Kujua zaidi kuhusu vigezo, tembelea kurasa yetu kuomba yaani Apply Page na Usome Jarida la Muombaji. Waliofikia hatua ya mwisho watatetea mawazo yao mbele ya jopo la majaji. Majaji hawa ni wataalam wazalendo ambao uendana na mada kuu zilizochaguliwa yaani themes. Kwa kutokana na maksi za majaji, washindi watachaguliwa kutoka kwa wale waliofikia hatua ya mwisho. Washindi ni lazima wapiti hatua ya kufanyiwa tathmini kabla ya kupatiwa ruzuku toka DLIIC.

Watu binafsi na timu ndogo ndogo wanaweza shinda mpaka Dola za kimarekani 25,000. Taasisi zilizosajiliwa zinawezashinda mpaka Dola za Kimarekani 100,000.

Fedha zinalenga  kusaidia kupata  ufanisi  katika kutafsiri wazo lako ndani ya suluhisho la ubunifu au bidhaa unayozungumzia  katika mawazo yako. Utahitaji kutoa ripoti ya maendeleo kuelekea lengo hilo na jinsi unavyoweza kutumia fedha kwa Meneja wa Misaada ya DTBi na / au mshauri wako wa ndani.

Mbali na kupokea pesa, washindi wataunganishwa na washauri katika maeneo yao. Mshauri huyu atasaidia katika kuendeleza mawazo yao ya ubunifu mpaka kuwa bidhaa iliyokamilika.

Utaweza kusaidiwa kuelezea na kushughulikia mahitaji ya Watanzania na kuboresha maisha na pia kupanga lengo lako , utekelezaji, usimamizi, ufuatiliaji na ujuzi wa kufanya tathmini. Kama mshiriki katika DLI Innovation Challenge, utakuwa pia na nafasi ya kukutana na kushirikiana na wavumbuzi wengine wa Tanzania, watengenezaji, wasaidizi wa takwimu na watoa huduma za kupatikana suluhisho.
Kuunganishwa na DLI Innovation Challenge inaweza kukupatia fursa za baadaye za kuboresha matumizi ya takwimu na kuondoa tofauti inayoonekana katika maisha ya watu.

Kwa wakati huu, DLIIC haitoi vyeti vya ushiriki kwa waombaji katika shindano. Tunakushauri utumie nakala ya maombi yako kama kithibitisho cha ushiriki wako katika shindano.

Zaidi ya utoaji wa ruzuku, DLIIC imelenga katika kuwashirikisha, kuwasaidia na kuwaunganisha watanzania wabunifu, wazalishaji na watoa tatuzi pamoja na na fursa ili kuleta utofauti chanya katika maisha ya watu kwa kuongeza matumizi na upatikanaji wa takwimu/data. Ungana nazi kupitia mitandao yetu ya kijamii na ujifunze vingi kuhusu matumizi ya takwimu/data na ujasiriamali, kuwaunganisha na wabunifu wengine, kusikia maoni toka kwa wataalam wengine, na kufahamu zaidi juu ya fursa nyingine za upatikanaji wa ruzuku.

JE UNA WAZO LA KIBUNIFU?