DLI yatangaza ubunifu wa Tanzania utokanao na data nchini Kosovo

DLI yatangaza ubunifu wa Tanzania utokanao na data nchini Kosovo

Agapiti Manday, Meneja wa mradi wa DLIIC, hivi karibuni alitembelea Kosovo na kuzungumzia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika nyanja ya ubunifu nchini Tanzania. Alishiriki katika uzinduzi wa #DigDataKosovo, shindano la wazi la data iliyoandaliwa na Taasisi ya Milenia ya Kosovo (MFK). Kama msemaji muhimu kwa uzinduzi wa shindano hilo, Bwana. Manday alishika jukumu muhimu katika kuhamasisha serikali ya Kosovo, wajasiriamali, na wataalam katika matumizi ya data kushiriki katika kujenga mazingira mazuri ya ubunifu.

Mbali na kuzungumzia juu ya mafanikio ya DLI nchini Tanzania, Bw. Manday alikuwa na ujumbe muhimu kwa waliohudhuria katika uzinduzi huo:

  • Kama Kosovo inapozindua shindano la ubunifu kutumia data, wanapaswa kutambua wanafanya jambo ambalo limeshafanyika huko Kosovo. DLI imethibitisha kuwa inawezekana kuendeleza ubunifu kupitia data nchini Tanzania.
  • Ubunifu unaotokana na data hauhitaji mara nyingi “teknolojia ya juu” kama vile akili ya bandia au blockchain. Inaweza kuhusisha bidhaa na vifaa vya msingi ambavyo vinatatua maeneo yenye changamoto katika jamii na hivyo hubadili maisha.
  • Wakati wa kuendeleza mazingira ya kibunifu, ni muhimu kujenga mitandao kati ya vijana, wabunifu na serikali, mashirika ya kiraia, na sekta binafsi.

Angalia zaidi kutoka kwenye uwasilisho uliofanywa na Bw. AgapitI Manday katika #DigDataKosovo:

Akizungumza baada ya kurudi kutoka Kosovo, Bw. Manday, alisema, “Ilikuwa ni heshima kubwa na utambulisho mkubwa sana kwa mradi wa DLI. Tulichaguliwa kushiriki katika Shindano la Open Data kwa sababu ya yale tuliyochangia katika sekta ya ubunifu nchini Tanzania. ”

Aliongeza “juhudi zetu na kazi ambayo tunasisitiza matumizi ya data katika ubunifu wa teknolojia ambazo zitakuwa na matokeo chanya kwa jamii zetu, zimekubaliwa na kwamba ni mafanikio kwetu kama DLIIC.

Wakati wa hotuba yake ya msingi katika tukio la uzinduzi wa shindano la wazi la data, Bw. Manday alipata fursa ya kuonyesha baadhi miradi ya kibunifu itokanayo na takwimu/data iliyoendelezwa na vijana wabunifu waliopata ruzuku kutoka katika mradi wa DLIIC.

“Walifurahi kuona jinsi gani tumepiga hatua katika eneo la ubunifu. Baada ya kuwaonyesha baadhi ya ubunifu uliofanywa na baadhi ya vijana waliofaidika na ruzuku kutoka DLI, walitambua ni aina gani ya ubunifu utokanao na takwimu/data wanaohuhitaji ili kuweza kufikia malengo yao, “alisema.

Ili kujifunza zaidi kuhusu miradi ndogo ya wafadhili wa DLI, angalia maelezo ya mshindi wa shidano la kwanza, la pili, na la tatu

Kuhusu Millennium Foundation Kosovo (MFK)

Taasisi ya Milenia Kosovo ni chombo cha utekelezaji wa mpango ujulikanao kama Threshold Program, ambao ni makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Kosovo na Taasisi ya Changamoto za Milenia. Mpango huo, unashughulikia vikwazo viwili muhimu kwa Ukuaji wa uchumi wa Kosovo: usambazaji wa umeme usioaminika; na udhaifu halisi na ulioonekana katika utawala wa sheria, uwajibikaji wa serikali na uwazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.