DLIIC yapata washindi wa awamu ya pili ya shindano la ubunifu

DLIIC yapata washindi wa awamu ya pili ya shindano la ubunifu

DLIIC yapata  washindi wa awamu ya pili ya shindano la ubunifu

Wabunifu tisa kutoka Tanzania  na taasisi moja isiyo ya kiserikali, Ubongo Kids, wapatiwa ruzuku ili kuwezesha utekelezaji wa  ubunifu wao kupitia mpango wa  Data for Local Impact Innovation Challenge (DLIIC) inayofadhiliwa na Mpango wa Dharura  wa  Rais wa Serikali ya Marekani  unaojihusisha na masuala ya  Ukimwi (PEPFAR) chini ya Ushirikiano wa  (DCLI)  wanaosimamiwa na taasisi ya kimataifa ya  Millennium Challenge Cooperation (MCC). Kwa kuteuliwa washindi  hao  watapata fedha  kuanzia  dola za Marekani 10,000 hadi 25,000 (watu binafsi) na dola 100,000 (kwa shirika) pamoja na msaada wa kiufundi na ushauri ili waweze kutekeleza  aina mbalimbali za ufumbuzi  wa  matatizo katika jamii.

Mnamo Oktoba 11  mwaka huu , DLIIC  itasherehekea na wabunifu hawa kama sehemu ya sikukuu ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike iliyoanzishwa mwaka huu na Umoja wa Mataifa ikiwa na kauli mbiu  “Nguvu ya Mtoto wa kike ikiwa na malengo ya hadi mwaka  2030”.

Dirisha la kwanza la DLIIC  lilifunguliwa  Oktoba  2016  likiwa na mapendekezo ya matumizi ya takwimu/Data ili kuweza kupata matokeo bora ya afya  na kusaidia katika vipaumbele vya afya vya Serikali ya Tanzania. Dirisha hili la pili  pia lilizingatia  vipaumbele vya afya vya Serikali ya Tanzania, na hasa kusaidia mipango ya kimkakati ya  PEPFAR   ili kushughulikia maambukizi ya VVU / UKIMWI kwa  watoto wa kike waliopevuka na wasichana vijana  (AGYW), ushirikiano unaojulikana kama DREAMS (Uamuzi, Ufanisi, Uwezeshwaji, epuka UKIMWI , Maelekezo, na Salama).

Ushirikiano wa DREAMS husaidia wasichana waliopevuka na wanawake vijana walio katika mazingira hatarishi wenye umri kati ya  miaka 10-24, ukilenga zaidi kwa wale wenye umri wa miaka 15 hadi 24. Kundi hilo ndilo liko katika mazingira hatarishi mara mbili nukta tano zaidi ya kuambukizwa VVU / Ukimwi  kuliko wenzao wa kiume. Ushirikiano huu wa DREAMS unalengo la kupunguza hatari hii kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana  na pia  kupunguza  maambukizi mapya ya VVU kati ya vijana hao wenye umri huo wa kati ya  miaka 15-24 kwa  asilimia 40 kupitia jitihada zenye vielelezo maalumu unaozingatia idadi ya watu katika makundi manne ambayo: wanawake vijana, watoa huduma, wapenzi wao, na washirika wao katika jamii. Hatua hizi zimeshibitishwa kupunguza tabia zinazosababisha uenezaji wa VVU  na unyanyasaji wa kijinsia (GBV).

Dirisha la pili la liliwalika waendelezaji wa ndani  ili kupata  ubunifu mpya, teknolojia, na taratibu zinazozotumia  takwimu  ili kushughulikia masuala yanayowakabili wasichana na wanawake vijana na kuchangia kupunguza maambukizi ya VVU.

Mapendekezo yaliyoshinda yalijumuisha ubinifu wa kupata suluhisho katika maeneo  yafuatayo:

  • Kuongezeka kwa ushiriki wa wanaume katika kujenga mazingira salama na kinga kwa Wasichana waliopevuka na wanawake vijana;
  • Kupunguza Uachaji wa shule ambao unapunguza fursa muhimu kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana;
  • Kupanua uwezeshaji wa kiuchumi na mikakati ya kuongeza uhuru wa kiuchumi kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana; na
  • Kuongeza uongozaji kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana na ufanyaji wa maamuzi katika kupambana na VVU.

Katika maeneo hayo mapendekezo kumi yalichaguliwa kutoka  katika maombi 190 baada ya kupitiwa na jopo  huru la la wajasiliamali wa kitanzania waliobobea katika masuala ya  afya, na wataalamu wa jinsia.

Mapendekezo yalitakiwa kuzalisha au kutumia  takwimu wazi na ziwe zimefanyiwa kazi   katika kipindi cha ndani ya miezi mitatu hadi sita  na kuzingatia masuala yanayowakabili vijana, wasicaha wadogo na jamii zilizopuuzwa. Ubunifu huo  pia ulitakiwa kulenga angalau moja ya wilaya 89 ambazo zinapewa vipaumbele chini  ya mpango wa  PEPFAR 2017 Tanzanian Country Operational Plan (COP)  au chini ya Mpango wa Mfuko wa Kimataifa ulioandaliwa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania. Mapendekezo yaliyoshinda, yameorodheshwa kwa kutaja viongozi wa timu na mada zao kuu, kama ifuatavyo;

Kuongezeka kwa usiriki wa wanaume katika kujenga mazingira salama na kinga kwa Wasichana waliopevuka na wanawake vijana;

  • Leyla Liana Hamisi
  • Mkata Nyoni

Kupunguza Uachaji wa shule ambao unapunguza fursa muhimu kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana;

  • Husseni Kiranga
  • Judith Leo
  • Maria Dorin Shayo
  • Wilson Mnyabwilo

Kupanua uwezeshaji wa kiuchumi na mikakati ya kuongeza uhuru wa kiuchumi kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana;

Kuongeza uongozaji kwa wasichana waliopevuka na wanawake vijana na ufanyaji wa maamuzi katika kupambana na VVU.

  • Asha Kombo
  • Emila Msangi
  • Musafiri Mbilinyi

“DLIIC  ina  lengo la kushiriki, kusaidia, na kuunganisha wabunifu  wa Kitanzania, watengenezaji, wavumbuzi na kufadhili  ili kila mmoja aweze kupata fursa za kufanya vitu tofauti  vinavyoyakabili maisha ya watu,” alisema Agapiti Manday ambaye ni  Meneja wa Programu  wa  DLIIC.

Alisema  DLIIC imeandaliwa kimkakati na ili kuwashirikisha   kikamilifu vijana katika  matumizi yao ya takwimu/data na  kuwajengea  uwezo  katika utumiaji wa data za kisayansi  na kuchangia lengo la PEPFAR  la  kuwa na ushiriki mkubwa kwa wananchi nchini  katika kudhibiti, na hatimaye kulitokomeza ugonjwa wa  UKIMWI.

Washindi wataanza mafunzo yao mwezi Oktoba 2017, na watafanya kazi  ya kutekeleza  miradi yao  ndani ya  miezi mitatu hadi sita. Washindi hao watakuwa sehemu ya mpango wa ujasiriamali ambao utaimarisha ujuzi wao wa usimamizi wa miradi, biashara  na watakuwa na uwezo wa kutumia data kisayansi. Jambo muhimu zaidi washindi hawa watasambaza maana halisi  ya kupatikana ufumbuzi wa matatizo yanayokabili maisha ya jamii ya Kitanzania  hasa wasichana  waliopevuka na wanawake vijana.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.